Unawajua Cannavaro, Boban, Nemanja Vidic, Garincha, Fabregas, Barthez wa Bongo? Wasome hapa
SOKA la Tanzania limekuwa likipiga hatua siku hadi siku na hiyo
inatokana na kuibuka kwa vipija vingi vya vijana ambao wanavutiwa na
mchezo huo unaoongoza kuwa na mashabiki wengi duniani.
Utaditi uliofanywa na Goal unaonyesha asilimia 65 ya vijana wa kiume
wa Tanzania wanapenda mchezo wa soka na wengi wao wamejiingiza kwenye
mchezo huo kama siyo kwa kuucheza basi kwa kushangilia timu mbalimba iwe
za ndani au za Barani Ulaya.
Kutokana na soka kuwa mchezo maarufu kupita yote duniani na ukiongeza
na utandawazi uliopo kupitia Televisheni hata wachezaji wakubwa
wanaocheza timu zinazo shiriki ligi kuu ya Vodacom wamekuwa ni
wafuatiliaji wa zuri wa ligi za Ulaya na wengine kutokana na uhodari
wame wamepachikwa majina ya utani ya wachezaji wa Ulaya na mashabiki wao
na wengine wamejipa wao wenyewe.
Hapa chini Mtandao wa Goal unakuletea wachezaji nane wenye umaarufu
mkubwa katika Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutumia AKA za majina ya wachezaji
wa Ulaya kiasi cha majina yao halisi kutofahamika kwa mashabiki.
1.Nadir Haroub ‘Cannavaro huyu ni nahodha wa klabu
kubwa Tanzania inayoongoza ligi kuu ya Vodacom na pia ni nahodha wa timu
ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutokana na nafasi anayocheza
uwanjani na mchango wake kwa timu hizo mbili amebatizwa jina la nahodha
wa timu ya taifa ya Italia Fabio Cannavaro.
Mchango wa Hadir Haroub kwa timu hizi mbili haupishani sana na
Cannavaro halisi wa Italia kwani amekuwa akicheza kwa bidii ya hali ya
juu na wakati mwingine ameweza kuifungia timu yake mabao mahimu katika
mechi muhimu na pindi anapokosekana labda kwa matatizo ya majeruhi ama
kutumikia adhabu basi hali huwa tete na hofu huongezeka kwa mashabiki
wake.
2.Haruna Moshi ‘Boban’ huyu ni kiungo mshambuliaji
wa timu ya Friends Rangars zamani aliwahi kutamba na klabu kubwa ya
Simba na hata Coastal Union alipewa jina la Boban na mashabiki wa SImba
kutokana na uwezo wake anapokuwa dimbani ambao ulikuwa ukifanana na ule
wa Mcroatia Zvonimir Boban aliyetamba na klabu ya AC Milani ya Italia.
Mbali ya uwezo wake awapo dimbani lakini Boban wa Tanzania amekuwa na
vituko vingi ambavyo vinamfanya awe mchezaji wakipee nchini na
haikushangaza Agosti 2010 alipovunja mkataba na timu ya Gavle IF, ya
Sweden aliyokuwa anaichezea kama Profeshino.
3.Kelvin Yondani , ‘Nemanja Vidic’ Huyu ni beki
mwingine mwenye jina kubwa kwenye ligi ya Tanzania bara akiichezea Yanga
na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ uwezo wake wa kuwadhibiti washambuliaji
hatari mashabiki wake wakati huo akiichezea Simba walimpa jina hilo
wakimfananisha na Vidic ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Inter Millan
ya Italia akitokea Mancherster United.
Sifa kubwa aliyokuwa nayo Yondan na kusababisha mashabiki hao
kumfananisha na Vidic ni jitihada zake anazozifanya uwanjani za kulinda
lango lake huku akiruka vichwa kwa kufunga au kuokoa kama ilivyo kwa
mwenye jina hilo Mserbia Nemanja Vidic .
4.Steven Mapunda ‘Garincha’ Huyu ni winga wa zamani
aliyewahi kutamba na klabu ya Simba na kidogo timu ya taifa ‘Taifa Stars
kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kupiga chenga akiwa kwenye kasi
mashabiki wa soka walimbatiza jina la Garincha akifanianishwa na
Mbrazili Manuel Francisco dos Santos
Uwezo wa mchezaji huyo aliyetamba na timu ya Brazili ulikuwa ni
hatari kwa mabeki wa timu pinzani sawa na Mapunda ambaye kwa sasa
ameshastaafu soka na yupo kwao Songea anaendeleza kipaji chake kwa
kuibua vipaji vya soka.
5.Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ Kiungo fundi raia wa
Rwanda anayecheza soka la profeshino kwenye klabu ya Yanga ya Tanzania
ni mmoja ya wachezaji maarufu Afrika Mashariki na Kati na kiwango chake
cha kuichezesha timu na kutoa pasi za mabao kumewafanya mashabiki wa
soka wa Rwanda kumpachika jina la kiungo huyo anayeichezea klabu ya
Chalsea ya Uingereza kwa sasa.
Uwezo wa Niyonzima mbaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda
‘Amavubi’ umeweza kuwavutia makocha wengi ambao wamekuwa wakimuhitaji
kwa ajili ya kuzitumikia timu zao na huenda mwishoni mwa msimu huu
kiungo huyo akaachana na Yanga na kurudi kwao Rwanda kuichezea APR kwani
amegoma kuongeza kusaini mkataba mpya.
6.Wazir Mahadhi ‘Mendieta’ Huyu ni kiungo wazamani
wa Tanzania aliyepata umaarufu mkubwa wakati akiichezea klabu ya Yanga
kutokana na uwezo wake mashabiki wa soka waliamua kumpa jina la kiungo
wa Hispania Gaizka Mendieta ambaye kwa sasa amestaafu soka .
Mara ya mwisho Wazir Mahadhi kuchezea timu za ligi kuu ya Vodacom
ilikuwa ni msimu wa 2009/2010, wakati aliposajiliwa na Moro United na
kuonyesha uwezo mkubwa pamoja na ukongwe aliokuwa nao lakini pamoja na
mchango mkubwa timu hiyo ilishuka daraja mwishoni mwa msimu na yeye
kuamua kustaafu rasmi kucheza soka.
7.Ally Mustaph ‘Barthez’ Huyu ni kipa changuo la
kwanza kwa sasa kwenye klabu ya Yanga ambaye uwezo wake wakati huo
akiichezea Ashanti ya Ilala 2006 ulisababisha mashabiki wa timu hiyo
kumpachika jina la Fabian Barthez kipa wa Ufaransa na klabu ya
Manchester United aliyefanya vizuri kwenye fainali za kombe la Dunia za
mwaka 1998.
Jina la Barthez limemsaidia sana kipa huyo wa Tanzania kudumu kwenye
soka kutokana na kupitia kwenye vipindi vigumu ikiwemo kukaa benchi kwa
msimu mzima wakati alipohamia Simba huku kipa namba moja wakati huo
akiwa Juma Kaseja, lakini uvumilivu wake ulikwisha baada ya kuhamia
Yanga misimu mitatu mitatu iliyopita na kuipa ubingwa Yanga katika msimu
wa kwanza lakini napo alipata matatizo baada ya kufungwa mabao matatu
dhidi ya timu yake ya zamani Simba na kuwekwa benchi kwa muda mrefu
kabla ya kupambana na kurudi kwenye nafasi yake.
8.Deogratius Munish ‘Dida’ Kama ilivyo kwa Batherz
Munish naye ni mmoja wa makipa hodari anayeichezea klabu ya Yanga na
timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ uwezo wake akiwa na klabu za
Simba, Mtibwa Sugar, Azam FC na sasa Yanga pamoja na urefu wake
mashabiki walimpachika jina la DIDA wakimfananisha na kipa wa Brazili
Nélson de Jesus da Silva aliyepata umaarufu mkubwa akiwa na klabu ya AC
Millan ya Italia.
Ingawa Dida wa Brazili kwa sasa hana jina baada ya kurudi kucheza
ligi ya kwao katika timu ya Sport Club Internacional lakini Dida wa
Yanga bado yupo kwenye kiwango licha ya kukosa namba kwenye kikosi cha
kwanza na hiyo ilitokana na uzembe alioufanya kwenye baadhi ya mechi na
kocha Hans van der Pluijm kumpa nafasi Barthez.
Utumiaji wa majina hayo kumekuwa kukiongeza hamasa kubwa kwenye mechi
za Ligi Kuu kwa sababu wachezaji hao wanalazimika kujituma zaidi
kuonyesha tofauti na wengine kutokana na kufahamika zaidi na wakati
mwingine kulinda heshima ya majina wanayoyatumia kwa kuonekana wapo juu
kila siku.