Sunday, September 29, 2013

SMBA MWENDO MDUNDO LIGI KUU BARA YAICHAPA JKT RUVU 2-0 UWANJA WA TAIFA

Simba sports club imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mashindano ya ligi kuu ya Tanzania bara inayojulikana kama Vodacom Primier league.

Timu hiyo ya simba imefanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Ilichukuwa dakika ya 25 pale beki wa jkt ruvu alipounawa mpira ndani ya eneo la hatari ndipo mwamuzi wa mchezo huwo kuamuru penalti ipigwe katika dakika ya 26.
Alikuwa mfmania nyavu maarufu tangu ligi kuu ianxe wa timu ya simba Amisi Tambwe alipokwenda kupiga penalt  na kuiandikia bao la kwanza  na kumuacha kipa wa jkt ruvu shabani dihile akiruka bila ya mafanikio.

Hadi mwamuzi anapiliza kipyenga kuamuru mchezo ni mapumziko na simba ilikuwa kifuambele kwa bao 1-0. Baada ya kipindi cha pili kuanza ilchukuwa dakika 30 tu ndipo mchezaji kinda wa timu hiyo ramadhan singano alipoingia kuchukuwa nafasi ya Amri Kiemba na kuiandikia goli la pili baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa mombeki.

Mpaka dakika ya mwisho wa mchezo huwo simba wakatoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0.

WAKATI HUO HUO:

Ligi hiyo iliendelea katika viwanja vingine ambapo katika uwanja wa sokoine mjini mbeya timu ya Azam alitoka sare ya nao 1-1 dhidi ya Prisons ya mbeya, pia katika uwanja wa chamanzi timu za mtibwa sugar na ashant united ya da es salaam walotoka sare ya mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment