STAA
wa filamu nchini na Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Isaac Sepetu,
amefiwa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu, aliyefariki
dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni mjini Dar es
Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Balozi sepetu wakati akitibiwa TMJ
Habari
zinasema kwamba, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital hiyo
akipatiwa matibabu ya magonjwa ya Kiharusi na Kisukari yaliyokuwa
yakimsumbua.
Balozi Isaac Sepetu amefariki akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. Pole Wema, pole familia ya marehemu ndugu na jamaa.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin.
No comments:
Post a Comment