Sunday, October 20, 2013

DANTE KUIKOSA PLZEN LIGI YA MABINGWA ULAYA

Beki wa kati wa kimataifa wa Brazil na timu ya soka ya Bayern Munich Dante anatarajiwa kuikosa mechi ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Plzen.

Nyota huyo aliumia katika mchezo wa ligi kuu ya ujerumani dhidi ya Mainz katika dakika ya 43 katika uwanja wa nyumbani ambapo kiungo Pospech alipomgonga mguuni katika harakati za kuokoa hatari ndani ya lango lao.

Dante atatarajiwa kukaa nje zaidi ya siku kumi akisuburia kupona maumivu hayo aliyo yapata guuni.

No comments:

Post a Comment