Thursday, October 31, 2013

MECHI YA SIMBA VS KAGERA SUGAR YAMALIZIKA KWA MABOMU

UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam leo uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu hizo zikitoka 1-1.
  Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani.

Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi.
  Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mohamed Theofile wa Morogoro aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, ambao walishindwa kuumudu kabisa, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Baadhi ya viti vilivyong'olewa leo na mashabiki
 Kipa wa simba akiongea na mwamuzi wa akiba
 Baadhi ya wachezaji wa simba katika huzuni
 Shabiki wa simba akiwa chini ya ulinzi
 Sehemu ya jukwaa likionyesha jinsi viti vilinyotolewa
 Salum kanoni mwenye rasta akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli la kusawazisha kwa njia ya penalti

No comments:

Post a Comment