Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Azam FC, umemalizika kwa Simba kufungwa bao 2-1.
Mabao yote mawili ya Azam FC yalifungwa na Kipre Tchetche, mshambuliaji kutoka Ivory Coast.
Ramadhani Singano ndie alieanza kuiweka Simba mbele kwa bao moja
bila, kabla ya Kipre kuisawazishia bao moja na baadae kuongeza la pili
la Ushindi.
Kwa matokeo hayo, Azam wanapanda nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 23.
Kapteni msaidizi wa timu ya simba Mganda Joseph Owino amesema kwamba ulikuwa ni mchezo mzuri ila haikuwa bahati yao kwa kuwa walicheza vizuri na kukosa nafasi nyingi katika mchezo huo na kuwa sisitiza mashabiki wa simba waskate tamaa na mchezo huu.
No comments:
Post a Comment