Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure
ameonesha kughadhabishwa na kulitaka shirikisho la kandanda barani
ulaya, UEFA kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ushangiliaji wenye
kuashiria ubaguzi wa rangi, baada ya kudai kuwa vilifanyika dhidi yake
timu yao ilipotoka na ushindi wa 2-1 jijini Moscow.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ivory coast
alisema alimlalamikia mwamuzi wa mchezo huo Ovidiu Hategan kuhusu
kitendo hicho, alipokuwa nahodha wa timu yake.
Toure anafikiri kuwa pengine shirikisho la soka barani ulaya litachukua hatua ya kufungia uwanja kwa miezi au miaka kadhaa.
Mwezi May, UEFA ilitangaza kuchukua hatua kwa
vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa rangi kwa kufungia kwa muda mfupi
viwanja iwapo ni kosa la kwanza, na kufunga moja kwa moja kwa kosa la
pili sambamba na adhabu ya kulipa pauni 42,800.
No comments:
Post a Comment