Mchezaji
maarufu wa timu ya Manchester City Yaya Toure, amewasili mjini Nairobi
Kenya kwa uzinduzi wa muungano mpya wa kukabiliana na uwindaji haramu
kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
mazingira (UNEP).
Muungano huo umeanzishwa ili kukabiliana na
uwindaji haramu wa wanyama pori haswa Ndovu ambao wanakabiliwa na tisho
la kudidimia kutokana na uwindaji haramu barani Afrika.
Toure, mshindi wa tuzo la mchezaji soka bora
zaidi Mwafrika kwa miaka miwili mfululizo, 2011 na 2012 ataeleza kwanini
amekubali kushirikiana na muungano huo kupambana dhidi ya uwindaji
haramu na nini hasa jukumu lake.
Anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa mataifa katika mtaa w akifahari wa Gigiri, Nairobi.
Wengine watakao zungumza ni Achim Steiner
mkurugenzi mkuu wa shirika la UNEP pampja na mkurugenzi wa shirikisho la
kandanda la kenya Sam Nyamwea.
No comments:
Post a Comment