Tuesday, November 6, 2018

TAIFA STARS YATUA SALAMA SOUTH AFRIKA KWA KAMBI YA WIKI 2

Taifa stars

Kikosi cha Stars kimewasili salama huko Afrika Kusini kwa kambi maalum kujiandaa na mechi dhidi ya Lesotho kuwania kufuzu AFCON 2019.


Wachezaji waliosafiri na timu ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Aaron Kalambo (Tz Prisons) Beno Kakolanya (Yanga SC) na Benedictor Tinocco (Mtibwa Sugar)

Mabeki ni Shomary Kapombe (Simba), Salum Kimenya (Tz Prisons) Erasto Nyoni (Simba) Ally ‘Sonso’ Abdulkarim (Lipuli) Kelvin Yondani (Yanga), Gardiel Michael (Yanga), Aggrey Morris (Azam) na Abdallah Kheri (Azam)

-Viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam) Mudathir Yahya (Azam) Feisal Salum Fei Toto (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shiza Kichuya (Simba). Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (Huru), John Bocco (Simba) na Yahya Zayd (Azam)

Aidha wachezaji wanaokipiga nje ya Tanzania wataungana na wenzao mbele ya safari tayari kwa mechi hiyo itakayopigwa Novemba 18.