Tuesday, February 18, 2014

AZAM NJIA NYEUPEEEE KWA KAPOMBE


WAKATI beki wa zamani wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Shomary Kapombe, anadaiwa kukataa kurejea katika timu yake ya AS Cannes ya Ufaransa, habari zaidi zimeelezwa kwamba wakala wake amewaambia Azam kuwa mchezaji huyo thamani yake ni Dola za Marekani 150,000. Habari kutoka kwa watu wa karibu wa mchezaji huyo zinasema kwamba nyota huyo amemueleza wakala wake, Denis Kadito, atakuwa tayari kurejea Ufaransa kucheza katika timu nyingine na si hiyo ya awali ambayo ilimpokea akitokea Simba.
Anarudi Ufaransa; Shomary Kapombe amekubali kurejea Ufaransa, lakini akachezee timu nyingine si AS Cannes

Chanzo cha gazeti hili kinaeleza kwamba tayari mazungumzo kati ya Kapombe na Azam yamefikia katika hatua za mwisho na ni moja ya sababu iliyomfanya beki huyo wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) kukataa kurejea Ufaransa. "Tayari Kapombe ameshamueleza wakala wake (Denis Kadito) kwamba hana nia ya kurejea AS Cannes, na hata kama akirejea Ufaransa iwe ni kwenye klabu nyingine," kilisema chanzo chetu. Hata hivyo, Kapombe, alikataa kuzungumza chochote kuhusiana na taarifa za yeye kukataa kurejea Ufaransa na kuelezea maamuzi yake ya kuendelea kukaa hapa nchini. "Kwa sasa siwezi kusema chochote, mtafute wakala wangu ndio atakayekueleza, nisamehe sana," alisisitiza beki huyo ambaye Simba ilimsajili akitokea Polisi Morogoro iliyowahi kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kwa sasa beki huyo anafanya mazoezi binafsi katika viwanja tofauti hapa jijini Dar es Salaam ili kulinda kiwango chake kisishuke. Afisa Habari wa Azam, Jaffer Idd, alisema kwamba ni mapema mno kuzungumzia usajili wa wachezaji katika muda huu ambao bado timu yao iko katika harakati za kuwania ubingwa wa Bara. Idd alisema kuwa muda muafaka utakapofika na dirisha la usajili litakapofunguliwa rasmi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndio wataanza zoezi hilo. Azam iliyokuwa inashiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho imeondolewa na Ferroviario de Beira baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 juzi huko ugenini. Kadito hakupatikana jana katika simu yake ya mkononi kueleza mikakati ya kumrejesha Kapombe Ufaransa kama ilivyotarajiwa baada ya kumaliza tofauti za mchezaji huyo na AS Cannes.

JANUZAJ AITWA KUICHZEA KOSOVO

KINDA Adnan Januzaj amepigiwa simu na Naibu Waziri Mkuu wa Kosovo kuombwa aichezee mechi ya kwanza ya kimataifa nchi hiyo.
Behgjet Pacolli, bilionea mmiliki kampuni za ujenzi anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 550, anajaribu kumshawishi Januzaj acheze dhidi ya Haiti mwezi ujao.
Januzaj, mwenye umri wa miaka 19, badohajaamua acheze nchi gani soka ya kimataifa, lakini familia yake ilikuwa moja ya wanaharakati wa uhuru wa nchi hiyo.
Wito Kosovo: Kosovo imemkaribisha mchezaji wa Manchester United, Adnan Januzaj aichezee timu yao ya taifa

Pamoja na hayo, Kosovo bado haijapata uanachama wa FIFA, wameruhusiwa kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Haiti mwezi ujao.
Januzaj alizaliwa mjini Brussels, Ubelgiji lakini kuna utata mkubwa juu ya mustakabali wake katika soka ya kimataifa.
England ni moja ya nchi ambazo zinatumaini kumpata Januzaj.
Breakthrough: Januzaj burst on to the Premier League stage with both goals in a 2-1 win at Sunderland earlier in the season
Tishio jipya: Januzaj alianza kutisha katika Ligi Kuu ya England mapema msimu huu kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 wa United dhidi ya Sunderland

HUYU NDIYO JOE MOURINHO AKIENDELEZA MDOMO WAKE HDIDI YA BARCA

KOCHA Jose Mourinho amewabwatukia Barcelona kuwatia presha kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo dhidi ya Manchester City.
Mwalimu huyo wa Chelsea, ambaye alishuhudia timu yake ikifungwa Uwanja wa Etihad katika Kombe la FA mwishoni mwa wiki, amesema Barca ya sasa ni mbovu mbovu ukilingalinganisha na miaka kadhaa iliyopita.
Cha mdomo; Jose Mourinho amesema Man City inakutana na Barca 'mbofu mbofu'
Leo ranger: Barcelona's Lionel Messi during a training session at the Etihad on Monday
Hasira za Leo: Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akiwa mazoezini Uwanja wa Etihad jana

Wakati kikosi cha Gerardo Martino hakiachani mbali sana na Real na Atletico Madrid katika mbio za ubingwa wa La Liga, lakini wanaonekana bado wapo imara katika michuano ya Ulaya.
Wametua Manchester jana asubuhi kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa. Licha ya kutemeshwa taji na mabingwa wa Ulaya wa sasa Bayern Munch msimu uliopita, bado wana nia ya kushinda tena mjini Lisbon. 
On the ball: Messi and Barcelona team-mates try out the Etihad turf
Messi na wachezaji wenzake wa Barcelona mazoezini Etihad
Cover up: Messi attempts to stay warm during a training session in Manchester on Monday

RATIBA: MICHEZO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WIKI HII

Tuesday 18 February 2014
Manchester CityvBarcelonaEtihad Stadium21:45
Bayer 04 LeverkusenvParis Saint GermainBayArena21:45 
Wednesday 19 February 2014 
MilanvAtlético de MadridGiuseppe Meazza21:45 
ArsenalvFC Bayern MünchenEmirates Stadium21:45