Saturday, September 21, 2013

AMIS TAMBWE AZIDI KUONYESHA CHECHE ZAKE SIMBA IKIVUTWA SHATI NA MBEYA CITY

Mshambuliaji wa kimataifa wa simba kutoka burundi Amis Tambwe ameendelea kuonyesha cheche zake baada ya kuendelea kufunga kila kukicha.

Mshambuliaji huyo leo tena katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara (Vodacom primer ligue VPL) dhidi ya mbeya city amefunga magili yote mawili ambapo timu yake ilitamgulia kupata na baadaye kusawazishwa.

Pia mshambuliaji huyo katika mechi ya jumatano alifanikiwa kupachika magoli 4 kati ya 6 ambayo timu ya yake iliipata na ushindi wa mabao 6-0.

Ligi hiyo iliiendelea tana leo na matokeo kamili ni:

simba 2-2 mbeya city

Tanzania Prisons 1-1 Mtibwa Sugar

Mgambo jkt  1-1 Rhino Rangers
 

Pia ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo wa mabingwa wa kombe hilo Yanga Sc watakapo kutana na Azam Fc katika uwanja wa taifa.
 

No comments:

Post a Comment