Wednesday, September 25, 2013

BAADA YA KUMALIZA ADHABU YA KUTOCHEZA MECHI 6 NGASSA ATAKIWA KULIPA FAINI ALIYOPEWA KUWA HURU

Winga machachari wa timu ya taifa ya Tanzania taifa stars na timu ya yanga sc Mrisho ngassa hatimaye memaliza adhabu aliyopewa na TFF kutocheza michezo6 ya ligi u ya tanzania bara VPL.

Lakini mchezaji huyo bado hayuko huru kwani bado anatakiwa alipe faini aliopewa ilikuwa huru, na kwa mujibu wa TFF anatakiwa alipe kiasi cha fedha.

Uongozi wa timu ya Yanga unasem bado wanamsikiliza ngassa kuhusiana na malipo ya faini hiyo ili aweze kutumiwa katika michezo ya ligi inayoendelea kwani yuko fiti na anafanya mazoezi na wachezaji wenzake kila siku.

Kwa mujibu wa maneno hayo inaelekea hata uongozi haujui nani atalipa ni yeye mwenyewe au uongozi utafanya maamuzi ya kumlipia. Kwa ushauri tu uongozi mlipieni kijana wenu ili acheze kwani yupo mikononi mwenu.

No comments:

Post a Comment