Kocha
wa Manchester United David Moyes amewaonya mashabiki wa mabingwa wa
ligi kuu ya England kwamba anahitaji kuimarisha kikosi chake na kwamba
kipigo cha Jumapili ambapo walichapwa 4-1 na Manchester City huenda
isiwe ndio mwisho wa matokeo kama hayo.
"Kutatokea
siku kama ile ya Jumapili na huenda tukakabiliwa na matokeo zaidi kama
hayo kwa sababu tuko katika kipindi cha mpito," aliwaaambia waandishi
habari kabla ya pambano la Jumaatano la kombe la Capital One dhidi ya
Liverpool.
"Tulihitaji wachezaji wawili watatu hivi ambao wangeweza kuingia moja kwa moja katika timu. Lakini hayo yatatokea, kweli huenda itabidi nikabiliane na vipigo vichache zaidi. Bado tunakabiliwa na kazi pevu ya kuwasajili wachezaji sio tu watakaojumuishwa na kikosi chetu lakini wenye uwezo wa kuingia moja kwa moja katika timu," aliongeza kusema Moyes katika msimu wake wa kwanza katyika a Old Trafford baada ya kushikikilia nafasi iliyoachwa na Alex Ferguson.
Manchester
United iliwakosa wachezaji kadhaa mastaa wakati wa kipindi kilichopita
cha usajili na hata kulikua na tetesi za juhudi za dakika ya mwisho za
kuipiku Real Madrid ili kumsajili Gareth Bale ambae kuuzwa kwake kutoka
Tottenham Hotspur kulivunja rekodi kama mchezaji ghali kupita wote
duniani.
Juhudi
za kuwasajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona, Ander Herrera kutoka
Athletic Bilbao na Fabio Coentrao kutoka Real Madrid ziliambulia patupu.
Leighton Baines aliamua kubaki Everton wakati Thiago Alcantara aliamua kuihama Barcelona na kujiunga na Bayern Munich.
Moyes
badala yake alikimbilia kumsajili mchezaji wa kiungo wa Ubelgiji
Marouane Fellaini, kutoka klabu yake ya zamani Everton, kwa dola
millioni ($43.96 ) dakika chache tu kabla ya kufungwa dirisha la
usajili.
No comments:
Post a Comment