Friday, September 13, 2013

MCHEZAJI CHELSEA AKUBALI KUICHEZEA TAIFA STARS

Mchezaji kinda wa timu ya chelsea mtanzania adam nditi hatimaye amekubali kichezea timu ya taifa tanzania taifa stars.

Kinda huyo aliyezaliwa zanzibar na alishawahi kuichezea timu ndoo ya kikwajuni ya unguja kwa sasa anacheza soka katika timu ya vijana ya chelsea.

Awali shirikisho la soka la tanzania lilijalibu kutaka kumjumuisha kinda katika timu za taifa hapa nchini ikiwemo timu chini ya miaka 20 lakini ilishindikana kutokana na tatizo la nyota huyo kukataa kuhofia uraia.

Lakini kwa sasa kwa mujibu wa baba wa mtoto huyo ameshatoa maelezo yote kuhusiana na mchezaji huyo kwamba hadi sasa ana passport ya tanzania pamoja na viza kwa hiyo anaruhusiwa kuichezea timu hiyo ikimuhitaji.

Inasemekana mchezaji huyo alienda england kwa ajili ya kusoma tu kwa kuwa alishindwa kusoma nchini na baba yake aliyekuwa anaishi huko tangia awali akaamua kumuamisha huko kimakazi. lakini kutokana na kupenda soka ndio ikamfanya siku moja aende kucheza mitaani na baadaye maofisa wa chelsea kumuona na kumsajili katika timu ya watoto.

No comments:

Post a Comment