Thursday, September 26, 2013

SIMBA YAJITOA KUWASILI KWA OKWI DAR NA KUSEMA KWAMBA HAWAHUSIKI NA KUJAKWAKE

Klabu ya simba ya tanzania imejitoa kuwasili kwa mshambuliaji wao wa zamani wa timu hiyo waliomuuza huko Tunisia katika timu ya etoel club dusaele Emmanuel Okwi na kusema kwamba hawahusiani na ujuo huo na hawana taarifa zozote.

Hayo yamekuja baada ya watu wengi wakizungumzia ujio wake ni kurudi katika timu hiyo kwa mara nyingine

.Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo msemaji mkuu wa timu hiyo ndugu Ezekiel Kamwaga alisema kwamba hakuna kingozi wa aina yeyote wa simba ambaye yuko karibu na ujio wa nyita huyo kutoka uganda

Vilevile Kamwaga alisisitiza kuwa watu waache kuvumisha habari za kwamba inasemekana simba imemrudisha nyota huyo na kuvunja mkataba na timu yake ktoka tunisia na kuja kujiunga na simba kwa mara nyingine.

Tena aliongeza ni kesi kubwa kuongea na mchezaji wa timu fulani aiwa bado anamkataba wa zaidi  ya miezi sita ili kumsajili.kwa hiyo okwi inawezekana amekuja dar es salaam  ni kwa kazi zake tu na sio kuja kwa ajili ya kujiunga na simba kani bado mchezaji huyo anamkataba na timu yake.

Hata hivyo simba bado wanawadai etoele dusahel dola 30000 ambazo bado simba hawajalipwa kutokana na usajili wa nyota huyo na simba walitarajiwa walipwe mwisho wa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment