Friday, October 4, 2013

EXCLUSIVE: TBC KUONYESHA MICHEZO YA LIGI KUU KUANZIA KESHO, BAADA YA KUPEWA RUHSA NA AZAM MEDIA

Shirika la utangazaji la tanzania kupitia television yake ya TBC1 huenda kuanzia kesho itaanza kuonyesha michezo ya ligi kuu ya tanzania bara maarufu kama VPL.

Shirika hilo limepata ruhusa hiyo kutoka kwa wamiiki wa haki hiyo AZAM MEDIA kupitia talevision yake AZAM TV.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati inayoendesha ligi hiyo amesema kwamba azam media imewapa ruhusa shirika hilo ilikuonyesha michuano hiyo huku wenyehaki ya kuonyesha ambao ni azam tv wakiwa wanakamilisha mambo yao vizuri ya kuwapa uondo washabiki wa soka na kusma kwamba kwa sasa mashabiki watapata uwondo huo kupitia TBC1 kwa muda na ikizngatiwa kwamba hatua zipo za mwisho kwa azam tv kuanza kuonyesha ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment