Saturday, October 19, 2013

JANUZAJ ASAINI MKATABA WA MIAKA MITANO MANCHESTER UNITED

Baada ya simulizi nyingi dhidi ya mkataba wa kinda chipukizi Adnan Januzaj hatimaye imefahamika kwamba kinda hilo limesaini mkataba wa miaka mitano katika timu hiyo.

Nyota huyo mwenye asili ya nchi za Albania,Belgium na Kosovo amesaini mkataba huwo utakaomfanyisha akae ndani ya timu hiyo hadi mwaka 2018 na kuzima mategemeo ya timu zinazomnyemelea kinda hilo.

Januzaj mwenye miaka 18 alifanya vizuri katika mchezo wa ligi kuu ya uingereza dhidi ya Sunderland na kufunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 na kuwashawishi viongozi wa timu hiyo akiwemo kocha Moyes na kumuongezea mkataba.

Kinda hilo ambalo hadi sasa hajaweka bayana timu gani ya taifa ambayo ataichezea kwani alisema ataweka bayana baada ya kusaini mkataba mpya na tusubiri atapendelea kucheza wapi?

"Nafurahi sana kusaini mkataba huu nadhani viongozi wamekuwa waelevu zaidi na nitahakikisha nacheza katika timu ya kwanza kwani nilikuwa natamani sana kuchezea timu hii katika maisha yangu ya soka na kuwa miongoni mwa wachezaji wakubwa duniani" alisema Januzaj.

United walimsajili kinda huyo mwaka 2011 akitokea Anderlecht ya Ubelgiji akiwa na miaka 16 na moja kwa moja kuanza katika kikosi cha kwanza cha vijana chini ya nyota wa zamani wa timu hiyo Ole Gunner Solskjier.

No comments:

Post a Comment