Monday, October 21, 2013

RATIBA LIGI KUU BARA YAPANGULIWA

Shirikisho la soka nchini Tanzania limepangua ratiba ya michezo ya ligi kuu bara kutokana na muingiliano na michezo ya kimataifa kwa timu ya tafa ya Tanzania ya wanawake chini ya miaka 20.

Shirikisho hilo limepeleka mbele michezo yote inayojumuisha raundi ya 11 na kuendelea ili kupisha mchezo wa timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake chini ya miaka 20 itakayo cheza dhidi ya Msumbiji tarehe na tayari timu hiyo ipo kambini na nwanja utakaotumiwa ni uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa TFF mechi za ligi hiyo raundi ya 11 itaanza kutimua vumbi mara baada ya kuisha mchezo huo na kuendelea ila raundi ya 10 bado ratiba yake ipo palepale ambapo mechi zake zitachzwa jumatano ya wiki hii.

No comments:

Post a Comment