MAKOCHA
watatu, Mromania Dorian Marin, Mcroatia Zdravko logarusic aliyewahi
kuifundisha Gor Mahia ya Kenya na Mtaliano Fabio Lopez, aliyewahi kuwa
Msaka Vipaji Mkuu wa klabu za Fiorentina na Atalanta za Italia, wameomba
kurithi mikoba ya Muingereza, Stewart Hall aliyeacha kazi Azam FC jana.
Habari kutoa ndani ya Azam FC, zimesema kwamba makocha hao wametuma wasifu wao na tayari unajadiliwa na uongozi na ambaye atawavutia ataitwa kwa mazungumzo.
“Atakayetuvutia tutamuita kwa mazungumzo, tukikubaliana ndiye atakuwa kocha mpya wa Azam FC,”kilisema chanzo.
ana,
Muingereza, Stewart John Hall aliwaaga wachezaji na benchi la Ufundi
mara tu baada ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara baina ya timu hiyo na Mbeya City ulioisha kwa sare
ya kufungana mabao 3-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
“Ni kweli nimewaaga wachezaji na wenzangu katika benchi la Ufundi, nimewaambia imebidi niondoke kwa sababu nimepata kazi sehemu nyingine. Lakini pia wamiliki wa timu wameridhia niondoke na ninaondoka vizuri, nawatakia kila heri,”alisema Stewart.
Hii inakuwa mara ya pili, Stewart kuondoka Azam, baada ya awali Agosti mwaka jana kuondolewa kiasi cha mwaka mmoja tu tangu aajiriwe akitoka kufundisha timu ya taifa ya Zanzibar.Stewart alifukuzwa baada ya kuiwezesha Azam kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu na Kombe la Kagame, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati pamoja na kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi na nafasi yake ikachukuliwa na Mserbia, Boris Bunjak.
Hata hivyo, baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu uliopita, Stewart aliyehamia Sofapaka ya Kenya, alirejeshwa Azam kufuatia kutimuliwa kwa Mserbia, Bunjak.
Stewart akarudia kuipa nafasi ya pili Azam katika Ligi Kuu na kuipa Kombe la Mapinduzi pamoja na kuiwezesha kutwaa taji la Ngao ya Hisani, michuano iliyofanyika mjini Kinshasa, DRC, Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment