Saturday, November 23, 2013

MICHAEL CARRICK IJITIA PINGU MAN UNITED HADI MWAKA 2015

KIUNGO Michael Carrick amesaini Mkataba mpya Manchester United, ambao utamfanya adumu Old Trafford hadi mwaka 2015.
 
Nyota huyo mwenye miaka 32 sasa amekuwa katika kiwango kizuri kwa muda wa miaka 3 sasa na imempelekea kuwepo katika kikosi cha kwanza katika kipindi chote hicho. Na mechi ya mwisho kwake ilikuwa dhidi yta Arsenal ambapo walitoka na ushindi wa bao 1-0.

Vilevile ni miuongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ya uingereza waliochaguliwa katika michezo ya kirafiki katikati mwa wiki iliyopita
 
Kiungo huyo kwa sasa yuko nje ya Uwanja kwa sababu ya majeruhi, lakini ameelezea furaha yake kwa kuongeza Mkataba na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.
 
Carrick amesema: "Ni babu kubwa kuongeza Mkataba wangu katika klabu hii kubwa. Hakika nafurahia soka yangu.

No comments:

Post a Comment