MWENYEKITI
aliyesimamishwa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage atarejea nchini Ijumaa
na kulakiwa na mamia ya wanachama na ataitisha Mkutano Mkuu, ambao
utafanyika Jumapili hii.
Na
katika Mkutano huo, Rage amepanga kuwasimamisha Wajumbe wote wa Kamati
ya Utendaji na baada ya hapo atasafiri kwenda nje ya nchi. Wajumbe wa
Kamati ya Utendaji waliobaki Simba SC ni Joseph Itang’are ‘Kinesi’, Said
Pamba, Ibrahim Masoud ‘Maestro’, Swedi Nkwabi na Zacharia Hans Poppe.
Habari
za kiuchunguzi zimesema kwamba, Rage
amekwishawasiliana na wafuasi wake wa Dar es Salaam na wameandaa
mapokezi makubwa kwake atakapokuwa anawasili Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam Ijumaa.
Baada ya hapo, Rage ataitisha Mkutano Mkuu wa dharula Jumapili na siku hiyo atawasimamisha Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji.
“Ni kwamba tumekwishajipanga na Mwenyekiti anarudi hapa Ijumaa na Jumapili unafanyika Mkutano Mkuu, Kinesi na wenzake wote nje,”alisema mmoja wanachama wanaomuunga mkono Rage ambaye kwa sasa yuko nchini Sudan kwa shughuli zake za kisiasa.
No comments:
Post a Comment