SERIKALI
ya Kenya imetoa dola za Kimarekani 125,000 (zaidi ya Sh. Milioni 140)
kudhamini michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Challenge inayoanza wiki ijayo mjini Nairobi.
Hili ni ongezeko la dola za Kimarekani 600,000 (zaidi ya Sh. Milioni 900) zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya Televisheni yatakayohusu mechi zote 27 za mashindano hayo.
Gavana
wa Machakos, Alfred Mutua naye ametoa Sh. Milioni 5 za Kenya zaidi ya
Sh. Milioni 11 za Tanzania kudhamini mashindano hayo, wakati wenzake
kutoka Nairobi na Kisumu wametoa Sh Milioni 10 za Kenya, zaidi ya Sh.
Milioni 22 za Tanzania.
Kampuni ya Coca Cola pia imetoa Sh Milioni 6.5 za Kenya (Milioni 5 taslimu na vinywaji vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5), wakati kampuni ya Bima ya UAP itatoa Sh Milioni 5.5 za Kenya (Milioni 2.5 fedha taslimu nan a Milioni 3 kwa ajili ya bima za wachezaji na marefa wote) katika mashindano hayo.
Kama ilivyothibitishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya, Sam Nyamweya, Serikali ya Kenya pia inakusanya fedha zaidi za kuongeza kwenye mashindano hayo na hivi karibuni itawasilisha mchango wake.
Michuano hiyo itafanyika katika miji mitano, Nairobi, Kisumu, Mombasa na Machakos kati ya Novemba 27 na Desemba 12, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment