Monday, November 25, 2013

YANGA WAMPIGA PINGU YONDANI, ASAINI MKATABA MPYA

KLABU ya Yanga SC imemuongezea Mkataba wa miaka miwili beki wake Kevin Patrick Yondan, ambaye alikuwa ananyemelewa na klabu yake ya zamani, Simba SC.

Yondan alisaini Mkataba huo juzi mjini Dar es Salaam na sasa atakuwa mali ya Yanga hadi Juni 2016.

Juni mwakani, Yondan alikuwa anamaliza Mkataba wake wa awali Yanga SC wa miaka miwili na kwa ndoa mpya- maana yake kuna uwezekano mchezaji huyo bora Mambo yanamuendea vizuri Yondan tangu ajiunge na Yanga SC, kwani mbali na kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, pia leo ameteuliwa kuwa Nahodha wa kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars. 
 
Kocha wa Stars, Kim Pouslen amemtambulisha Yondan kuwa Nah
odha mpya wa timu hiyo, anayechukua nafasi ya Juma Kaseja aliyeachwa kwenye kikosi hicho kinachoondoka jioni ya leo kwenda Nairobi, Kenya kushiriki michuano ya Kombe la Challenge inayoanza kutimua vumbi Novemba 27 mwaka huu.
Stars imeagwa leo mchana kwa hafla fupi kambini kwao katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa bendera na Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya.wa Ligi Kuu msimu uliopita atamalizia soka yake Jangwani.

No comments:

Post a Comment