Mpendwa Moyes,
Kwa
heshima na taadhima juu ya ukweli kwamba uliteuliwa na Sir Alex
Ferguson, ningependa kutoa maoni namna nisivyoridhishwa na unavyoendelea
kuiharibu ngome ambayo ilituchukua miaka mingi kuijenga.
Kwanza,
kuhusu mchezo dhidi ya Everton, haikuwa siri kwamba Fellaini, Giggs na
Wellbeck hawakuwa na msaada kwa timu… huzuni ni kwamba Kagawa na Rafael
wakawa wahanga wa ile 'small team mentality' ambayo inaonyesha wazi ni
vigumu kuiondoa kichwani mwako!! Ukamuingiza Chicharito dakika za
mwisho ili nae akumbane na aibu uliyotuletea.
Ikiwa
bado hujajua, wewe sasa ni kocha Manchehester United na utamaduni wa
Manchester united hatuchezi ili kushinda tu mechi kadhaa bali ni
kushinda ubingwa wa ligi.
KUTOKA KWENYE MTAZAMO WA KIJAMII
Je
una ufahamu wowote namna ulivyotutengenezea mazingira magumu sisi
mashabiki wa (MAN UTD) kuvaa jezi zetu za MAN UTD?? Unajua namna ambavyo
tunaepukana na mitandao ya kijamii kwa kuogopa madongo na maneno ya
kejeli ya wapinzani wetu? Nina uhakika ulisikia, wakati ukiwa Everton
kwamba sisi tuna kelele na tunaongea sana kuhusu ubora wa yetu lakini
mpaka sasa hautupi msingi wa kuweza kuizungumzia timu yetu kwa mazuri,
unatupa unyonge ambao hatujauzoea.
MTAZAMO WA KIUCHUMI
Jaribu
kufikiria kuhusu wale wenzetu ambao huwekeza fedha zao katika michezo
ya kubet ambao sasa wengine wanafilisika kutokana na timu kufanya
vibaya.
Angalia
namna mapato ya baa na migahawa yanavyoathirika kwa sababu wengi wetu
mashabiki wa United tunaangalia mpira tumejifungia majumbani mwetu.
Nafahamu unajua wengi wetu tunakunywa sana.
MTAZAMO WA KIIMANI.
Vitabu
vya dhambi zetu hivi sasa vimezidi kuisha kurasa kwa sababu umetufanya
tumekuwa tunatukana sana siku hizi, kutabasamu kwetu imekuwa tatizo na
badala yake presha zetu zinaishia kwa wake zetu, watoto wetu na watu
wetu wa karibu wasio na hatia.
MTAZAMO WA KIAFYA
Maisha
yetu ya siku hizi yamekuwa kama wagonjwa wa "Insomnia" (Ugonjwa wa
ukosefu wa usingizi) wiki mpaka wiki, wengi wetu mashabiki wa Man UTD
sasa tumekuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya presha kwa msongo wa
mawazo unaotupa, pia unajua madaktari wengi ni mashabiki wa Man UTD
hivyo unaweza ku-imagine namna wagonjwa ambao ni mashabiki wa Arsenal,
Chelsea na Liverpool wanavyokuwa katika wakati mgumu kutibiwa vizuri
(especially in the theatre)
Nakataa
kuamini kwamba sisi ni timu ndogo kwa sababu tumekuwa tukitafuna bubble
gum na kubeba tu makombe. Tumegoma kutumia mikono yetu yote miwili
kuhesabu tofauti ya pointi zilizopo baina yetu na viongozi wa msimamo wa
ligi. Tumegoma kuona ukiwaacha wachezaji wa maana kwenye benchi na
kufanya majaribio yako na Fellaini(Nyoshi), Giggs na Welbeck.
Nakutakia
kheri ukiwa unaanza vita ya kupigania ajira yako ndani ya old Trafford
na ningependa kukushauri kwamba jaribu kutafuna bubble gum, utaonekana
vizuri kiasi.
P.S: Hongera kwa kutimiza lengo lako; Kuifunga Man UTD ndani ya old Trafford na kutibua rekodi yetu.
Kwa huzuni kubwa na masikito,
Ni mie mshabiki mkubwa Man UTD
No comments:
Post a Comment