Saturday, December 14, 2013

BREAKING NEWS: VAN PERSIE NJE MWEZI MMOJA, BAADA Y KUUMIA DHIDI YA SHAKHTAR JUMANNER

Kocha wa mabingwa watetezi wa ligi kuu England David Moyes amebainisha kwamba timu yake itakosa huduma ya mshambuliaji wake tegemezi Robin Van Persie kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Kocha huyo amesema kwamba mshambuliajihuyo alipata majeruhi hayo baada ya kujaribu kufunga mpira wa kona katika mechi dhidi ya Shakhtar Donesk jumanne iliyopita.

Kwa mujibu wa madaktari wa timu hiyo wamesema kwamba RVP amepatwa na tatizo la taya na atakuwa nje kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Akilizungumzia swala hili kocha wa timu hiyo Moyes amesema kwamba ni pigo kubwa hasa ukifikiria timu ipo nyuma ya point 13 dhidi ya kinara wa ligihiyo Arsenal na isitoshe alishatoka katika majeruhi na alicheza mechi moja tu ya ligi wiki iliyopita na United kufungwa 1-0 na Newcastle.

Vilevile aliongezea kwamba kwa sasa hana budi kwa kuwa huwa anamtegemea sana katika safu ya ushambuliaji kwa kumuunganisha na nyota wa timu hiyo Rooney.

No comments:

Post a Comment