Pamoja
na kufungwa ugenini magoli 2 - 1 na TP Mazembe ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Club Sportif Sfaxien ya Tunisia imenyakua kombe
la shirikisho barani Afrika kufuatia kushinda mechi ya mkondo wa awali
kwa jumla ya magoli 2 - 0.
Mechi hiyo ya fainali mkondo wa pili imechezwa kwenye uwanja wa Lubumbashi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hata hivyo jitahata zao za kutaka kunyakua kombe
hilo kwa mara ya kwanza zilizimwa katika ya 88 baada ya Fakhereddine
Ben Youssef wa CS Sfaxien kupachika goli zuri kwa kichwa.
Hadi mwamuzi anapuliza fililmbi ya mwisho TP Mazembe ikawa imeifunga CS Sfaxien magoli 2 - 1
Kwa matokeo hayo na yale ya mkondo wa kwanza wa fainali hiyo CS Sfaxien ikawa imeiadhibu TP Mazembe kwa jumla ya magoli 3 - 2.
CS Sfaxieni wananyachukua kombe hilo kwa mara ya
tatu baada ya kulinyakua mwaka 2007 na 2008 . TP Mazembe ilikuwa
ikijaribu kunyakua kombe hilo kwa mara ya kwanza lakini ndoto hizo
zimezimwa na Club Sportif Sfaxien.
TP Mazembe pamoja na kushindwa kunyakua kombe
hilo la shirikisho barani Afrika, imeshanyakua kombe la Klabu Bingwa
bara Afrika kwa mara kadhaa.
Mshindi wa kombe hilo Club Sportif Sfaxien ya
Tunisia pamoja na kunyakua kombe hilo pia klabu hiyo imepewa kitita cha
dola za kimerekani 660,000 ambazo ni zawadi kwa bingwa wa kombe hilo.
Vile vile CS Sfaxien itakutana na Klabu Bingwa barani Afrika Ahly ya Misri mwaka kesho katika kombe la maalum la "CAF Super Cup"
No comments:
Post a Comment