Everton Ribeiro amekaririwa akisema atafurahia kipata nafasi ya kujiunga na Manchester United.
United
wameonyesha kuvutiwa na Ribeiro ambaye aliisaidia Cruzeiro kushinda
ubingwa wa Brazil na alitajwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo msimu
unaoisha hivi sasa.
Cruzeiro
wanataka kiasi kisichopungua £10million kwa ajili ya kiungo huyo mwenye
umri wa miaka 24 ambaye pia anahusudiwa na Liverpool.
Ribeiro
aliiambia ESPN Brasil: ‘United wana Kagawa, Rooney, De Gea ni golikipa
mzuri. Nawajua vizuri kwa sababu ninawauatilia na pia nachezea sana timu
hiyo kwenye video games kwasababu ni timu nzuri.
‘Nahisi
nipo tayari kucheza popote pale duniani. Ikiwa unachezea Cruzeiro, basi
unaweza kucheza popote pale. Naweza katika nafasi yoyote katika eneo la
kiungo. Nacheza vizuri pia katika kusaidia mashambulizi.’
Alipoulizwa
kama atakuwa akicheza pamoja na Robin van Persie na Wayne Rooney,
kiungo huyo alisema: ‘Itakuwa jambo zuri sana. Namuachia wakala wangu
na Cruzeiro kuzungumzia juu ya suala hilo. Ikiwa wataona ni jambo la faida kwetu sote, watanifahamisha."
No comments:
Post a Comment