WINGA
Gareth Bale jana amefunga mabao matatu peke yake yaani hat-trick wakati
Real Madrid ikiitandika Valladolid 4-0 Uwanja wa Bernabeu, Madrid na
kuisogelea Barcelona kileleni mwa La Liga ikibaki inazidiwa pointi tatu.
Mchezaji
huyo ghali wa dunia ameendelea kutekeleza vyema majukumu ya Cristiano
Ronaldo ambaye ni majeruhi kwa sasa akiwa ametimiza mabao tisa katika
mechi 13.Bale aliyefunga mabao hayo katika dakika za 33, 64 na 89 huku
lingine liifungwa na Karim Benzema dakika ua 36, anakuwa mchezaji wa
pili wa Uingereza kufunga hat-trick katika La Liga akimfuatia Gary
Lineker mwaka 1987.
Real Madrid: Lopez, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Alonso, Modric, Di Maria, Isco, Bale na Benzema.
Real Valladolid: Marino, Alcatraz, Rueda, Valiente, Pena, Rubio, Sastre, Rossi, Larsson, Guerray na Bergdich.
La kwanza: Winga wa Real Madrid, Gareth Bale akishangilia bao lake la kwanza Uwanja wa Bernabeu jana
Bale akimtoka mshambuliaji wa Valladolid, Javi Guerra
Bale ameisaidia Real Madrid kupunguza la pointi La Liga wanazozidiwa na vinara Barcelona hadi kubaki tatu
No comments:
Post a Comment