Monday, December 23, 2013

MPUTU AMUACHIA MIKOBA SAMATA TP MAZEMBE YEYE ATIMKIA ANGOLA


Mchezaji nyota zaidi wa TP Mazembe, Trésor Mputu ameondoka katika klabu hiyo na kutua nchini Angolan kuichezea Kabuscorp.
 Radio Okapi ya DR Congo imetangaza leo mchana kwamba Mputu amejiunga na klabu hiyo kwa kitita cha euro milioni 2 ambayo ni rekodi ya usajili na atakuwa akilipwa kitita cha euro 40,000 kwa mwezi.
Kuondoka kwa Mputu TP Mazembe, maana yake tegemeo anakuwa Mtanzania, Mbwana Ally Samatta ambaye amekuwa kipenzi kikubwa cha mashabiki wa timu hiyo baada ya Mputu.
Lakini mtandao wa TP Mazembe haukuthibitisha lolote kuhusu hilo na taarifa yake ya mwisho iliyotundikwa mtandaoni juzi imesema:  “Kutokana na taarifa za mitandao mingi kuwa Mputu anakwenda Angola, ukweli bado kila kitu hakijawa wazi na kama kuna ofa klabu inazisubiri kwa hamu kubwa:”
Mputu hakuonekana kambini baada ya Kocha Santos Mutubile kuita wacheza wa timu ya taifa ya DRC maarufu kama Leopards kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka.
Lakini baadaye ilielezwa alisafiri kutoka Kinshasa hadi Luanda, Angola na kupokelewa na mashabiki kibao wa Kabuscorp kwenye uwanja wa ndege na baadaye akasaini mkataba wa mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment