MSHAMBULIAJI Luis Suarez ametajwa mchezaji bora wa mwaka wa tuzo ya Shirikisho la Mashabiki wa Soka jana usiku.
Kiasi
kisichozidi miezi sita baada Arsenal kutaka kumnunua kwa Pauni
40,000,001 nyota huyo wa Uruguay, Suarez aliinua tuzo hiyo Emirates.
Lakini
ilikuwa ni tuzo binafsi kwa mshambuliaji huyo wa anayemtoa udenda kocha
Arsene Wenger, akiwapiku Leighton Baines, Christian Benteke, Juan Mata,
Robin van Persie na Pablo Zabaleta kushinda tuzo hiyo iliyohusisha
wapiga kura zaidi ya 500,000.
Mshindi: Mchezaji Bora wa Mwaka, Luis Suarez akisherehekea tuzo yake ya Shirikisho ya Mashabiki wa Soka, akiwa na mkewe Sofia
Mshambuliaji
huyo wa Liverpool, aliyehudhuria shughuli hiyo Emirates, alisema:
"Nafikiri ni haki kusema mwaka uliopita ulikuwa mzuri kwangu.
"Tuzo
hii si yangu peke yangu, ni pamoja na wachezaji wenzangu, uongozi na
benchi la Ufundi na yeyote anayehusiana na Liverpool,".
Suarez akisherehekea na tuzo yake Uwanja wa Emirates
No comments:
Post a Comment