Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jana ilipandishwa virago na kurejea Tanzania baada ya kupokea vichapo vitatu mfululizo kutoka kwa swazland,madagascar na lesotho.
Timu hiyo dhaifu kuwahi kutokea katika michuano hiyo aambayo walienda kushiriki kama waalikwa wakiwemo na timu ya taifa ya Ghana. Stars alioongozwa na Cap[tain wao John Bocco baada ya kuchukua kitambaa hiko kutoka kwa Nadir Haroub amabaye ni majeruhi.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanasema kwamba timu hiyo si ya taifa ni TFF kwani uteuzi wake ulifanywa kwa magumashi na kutoangalia uwezo wa mchezaji katika ligi iliyoisha hivi karibuni.
Kuna wachezaji wengi ambao wameonyesha kiwango kikubwa kama Salum Telela, Jonas Mkude, Hassani Kessy, Malimi Busungu, Rashidi Mandawa, David luhende na wengineo wengi ambao wameonyesha kiwango kizuri, cha kushangaza wachezaji hao hawakuitwa na matokeo yake wameitwa wachezaji majeruhi na walioshuka kiwango hivi karibuni mfano, Kazimoto, John Bocco, Saidi juma, oscar Josha, Erasto Nyoni,.
Kwa mujibu wa mashabiki walioambatana na timu hiyo huko Afrika Kusini, wanasema kwamba sababu ya timu hiyo kufanya vibaya ni kutokuwa na ushirikiano baadhi ya viongozi walioambatana na timu hiyo na kwamwe timu haiwezi kufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment