Angel Di Maria amekanusha tetesi
zinazoeleza kuwa yupo katika mpango wa kutimka Manchester United na
amesisitiza kuwa atarudi Old Trafford msimu ujao.
Nyota huyo wa kimataifa wa
Argentina alijiunga na Man United kwa ada ya usajili ya paundi milioni
59.7 akitokea Real Madrid na kuvunja rekodi ya usajili nchini Uingereza,
lakini ameshindwa kuonesha cheche katika msimu wake wa kwanza.
Di Maria ambaye yupo na timu ya
taifa ya Argentina inayocheza michuano ya Copa America amesema hana
mpango wa kuondoka Man United na anatarajia kurudisha kiwango chake
msimu ujao chini ya Louis van Gaal.
“Nimemaliza msimu wangu wa kwanza
kuichezea Manchester United,” Amewaambia The Sun. “Ulikuwa msimu mgumu
kwangu. Nadhani ulikuwa mgumu kwasababu ilikuwa ni taifa lingine na
klabu nyingine, ligi hii ni ngumu kuliko ya Hispania. Sikuweza kuendana
nayo kwa haraka”.
Sasa nitacheza Copa America na kurudi kucheza Manchester United msimu wangu wa pili, nadhani nitarudi kwenye ubora wangu”.
Kiufupi tu ni kwamba Angel Di Maria amefanikiwa kuchukuwa tuzo baada ya goli lake alilofunga dhidi ya Liecester City kuchaguliwa kuwa gili bora la msimu baada ya kumpiku Chalie Adam na goli lake alilofunga dhidi ya chelsea kwa msimu uliopita wa ligi 2014-2015. .

No comments:
Post a Comment