TFF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano wa klabu ya Simba.
TFF imeagiza mwakilishi wa klabu
ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne
tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo.
Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.
Katika kipindi hiki cha kuelekea
kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa
matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya
katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment