Mlinzi wa zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars,) Lubigisa Madata Lubigisa amesema kinachoendelea katika
klabu yake hiyo ya zamani ni ‘matokeo ya ubinafsi na kutowajibika
ipasavyo’ kwa uongozi wa juu ambao kwa mawazo yake (Lubigisa)
wameshindwa kuwa karibu na wachezaji na kutowatimizia mahitaji yao
muhimu.
Madata ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichofuzu kwa
hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2003 amesema hayo
wakati nilipomuomba mtazamo wake kuhusu mwenendo wa timu hiyo inayosotea
taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo hivi sasa.
“Kinacho endelea Simba sasahivi ni maslahi binafsi ya viongozi.
Viongozi wanajali sana maslahi yao binafsi na kusahau kama jukumu lao la
kuifanya Simba ishinde, kiongozi aliye makini tena wa club kubwa kama
Simba anaye hitaji matokeo mazuri ili aongoze ligi hawezi kukubali
kufungwa na Toto.”
“Ninachokiona kwa uongozi ni hawataki kutumia pesa ili washinde mechi
kama ile, kiongozi lazima uwe karibu na wachezaji wako tumia pesa kwa
wachezaji wako waahidi pesa ili wacheze kwa moyo na kujituma zaidi.”
No comments:
Post a Comment