Sunday, August 4, 2013

SAKATA LA YANGA KUGOMEA HAKI MILIKI KWA AZAM TV KUONYESHA LIGI KUU BARA

Kutokana na upeo wangu katika maswala ya soka hadi hivi sasa , ili ujulikane kitaifa na kimataifa lazima utangazwe katika vyombo tofauti vya habari na ndio watu mbalimbali watakujua ww ni nani katika hii dunia ya soka ,na sio soka tu bali hata nyanja zingine za mafanikio.

 Kutokana na watu a azam media kulijua hili wakaona ni bora ligi yetu kwa sasa muda umefika ili itangazike duniani na kwa kila mtu ifikie tamati amjue mchezaji wake kutoka timu husika kama tunavyoona ulaya kwani hivi sasa tunaweza kumjua mtu kama torres,ronaldo, messi hata akipita leo kwenye mitaa ya kariakoo watu humjua na vivyo hivyo kwetu muda umefika bwana  ligi yetu inatakiwa ionekane kote hata kwa afrika inatosha ili wachezaji wetu wapate soko katika timu za  ulaya

 Na sio hivyo tu bali hata vilabu vyetu vidogo vipate fedha za kujikimu kipindi chote cha ligi, sasa mimi na shangaa hawa viongozi wa yanga wanaleta masilahi yao binafsi kuliko masilahi ya timu zote katika ligi mimi naamini kwa kiasi ambacho azam tv kitatoa kitawasaidia sana timu zingine ambazo hali yao kifedha ni tata kuliko kukataa na kukubali laki moja kwa kila mchezo ambao utachezwa kama ilivyo zoeleka
.
Sasa naiomba timu ya yanga ikubali na ifikirie kwa jicho lingine wasilete itikadi zao za kibiashara  kwenye soa letu .

No comments:

Post a Comment