Baada
ya vuta ni kuvute huku ikitishiwa kulimwa adhabu na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), klabu Yanga imekubali matokeo na kumalizana na wachezaji wake wa zamani, Stephano Mwasika na Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ waliokuwa wakiidai klabu hiyo zaidi ya Sh15 Milioni.
Tanzania (TFF), klabu Yanga imekubali matokeo na kumalizana na wachezaji wake wa zamani, Stephano Mwasika na Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’ waliokuwa wakiidai klabu hiyo zaidi ya Sh15 Milioni.
Wachezaji
hao walikuwa wanaidai Yanga fedha hizo kutokana na malimbikizo ya ada
ya usajili, ambapo uongozi wa klabu hiyo ulikuwa ukiwapiga danadana
kuwalipa wakati walipokuwa waikiitumikia.
Kutokana
na hali hiyo wachezaji hao baada ya kuachwa na klabu hiyo katika
usajili wake wa msimu huu waliamua kuishtaki Yanga ili iweze
kuishinikiza na kuwalipa haki zao.
Nsajigwa,
alikuwa akiidai Yanga kiasi cha Sh 9 milioni wakati Mwasika ambaye sasa
anaitumika Ruvu Shooting alikuwa akiidai Yanga Sh 6.5 milioni.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameliambia gazeti hili jana kuwa wamemalizana na wachezaji hao siku tatu zilizopita.
Alisema
Yanga haikuwa na nia ya kuwadhulumu wachezaji hao isipokuwa malipo yao
yalichelewa kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali za kiutawala.
“Tumemalizana nao, lakini ni vema ukawauliza na wenyewe kwa uhakika zaidi,” alisema Mwalusako.
No comments:
Post a Comment