Friday, September 27, 2013

WENGER AJIANDAA KUSAINI MKATABA MPYA NA ARSEAL

Kocha mfaransa  anayefundiaha timu ya arsenal kwa muda mrefu ArsenE wenger anatarajiwa kuongeza au kusaini mkataba mpya na timu hiyo hivi karibuni.

Mfaransa huyo mwenye miaka 63 sasa anatarajiwa kuongeza mkataba utakaomfanyisha akae klabuni hapo kwa muda mrefu.


Awali kocha huyo alitangaza kutoongeza mkataba na timu hiyo na hata kufuatia tetesi za kuhamia timu ya real madrid ya hiapania ili kuifundisha,


Lakini kutokana na supoti kubwa kutoka kwa mmiliki wa timu hiyo Stan Kroenke sasa wenger anatarajiwa kuongeza mkataba wa kuwepo zaidi klabuni hapo.

Wenger na arsenal wana mkataba ambao utaishia msimu huu na ndio maana mmiliki wa timu hiyo anatarajia kukaa na wenger ili kuzungumza kuhusianan na kuongeza mkataba wa kuifundisha timu hiyo ambayo kwa sasa imeanza vizuri katika kampeni zake za kutaka kunyakuwa ubingwa wa uingereza.

No comments:

Post a Comment