Friday, September 20, 2013

LIONEL MESSI NA NDOTO ZA KUTAKA KUVUNJA REKODI YA RAUL LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na clubu ya barcelona ya hispania lionel messi anatarajia kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa magoli katika ligi ya mabingwa ulaya kwa kipindi chote.


Hadi hivi sasa anayeshikiria rekodi hiyo ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya hispania na clabu ya real madrid raul gonzalez kwa magoli 71.

Na sasa messi anafuatia akiwa na magoli 62 na bado yupo kwenye mchezo na anatarajiwa kuvunja rekodi hiyo mwaka huu kama akiendelea na moto aliouwasha jumatano kwa kupachika magoli matatu dhidi ya ajax amsterdam ya uholanzi na barcelona kutoka na ushindi wa mabao 4-0.ndani ya camp nou.

No comments:

Post a Comment