Saturday, September 7, 2013

RAY C ASEMA KWELI

Msanii huyo ametamka kwamba mpenzi wake aliyekuwa anaishi naye Kenya ndiye tatizo na ndiye aliyemlazimisha na kumuingiza kwenye dawa za kulevya na hata mamilioni ya fedha aliyokuwa akipata huko na yenyewe yalikuwa ni tatizo kubwa pia kwani alishindwa kujimudu.


RAY C ambaye amekiri kwamba sasa angalau amepona na anaendelea vizuri ametoa ushuhuda mzito kuhusu sakata lake la dawa za kulevya.

Msanii huyo ametamka kwamba mpenzi wake aliyekuwa anaishi naye Kenya ndiye tatizo na ndiye aliyemlazimisha na kumuingiza kwenye dawa za kulevya na hata mamilioni ya fedha aliyokuwa akipata huko na yenyewe yalikuwa ni tatizo kubwa pia kwani alishindwa kujimudu.“Awali sikujua ni wanaume wachache wanaoingia kwenye uhusiano wa mapenzi ya kweli waliobaki ni kwa faida zao, nilipopata matatizo ndiyo nikagundua kuna wanaume wanawatumia wanawake kwa faida yao, kama si uhusiano, inawezekana nisingekuwa Ray C huyu unayezungumza naye, ambaye inabidi apambane na unene, atafute pumzi ya kuimba upya.

 Lakini uhusiano wa kimapenzi na mwanamume niliyeamini ananipenda ndiyo ulionifikisha hapa bila kujua.”“Wasichana hasa maarufu wawe makini na wapenzi wanaoishi nao bila kujali wameishi nao kwa muda gani, wengi wao ni chanzo cha kufeli kwao kimaisha.

Nilikuwa nafanya kazi Nairobi napata Sh.10 milioni kwa mwezi, zote ziliishia kwenye dhambi.??Kwa tamaduni za Kiafrika wanawake tunawasikiliza wanaume, tunaonyesha unyenyekevu kwao, kumbe wakati mwingine wanatuingiza katika majanga. Sitaki kumtaja aliyeniingiza katika hii dhambi, lakini ni mpenzi wangu niliyempenda na alifanya hivyo bila mimi kujua.

Nawataka hata vijana wa kiume wawe makini na uvutaji sigara au bangi, kwani wakati mwingine wanachanganyiwa na dawa za kulevya na matokeo yake wanakuwa mateja.
“Wauza bangi wengi wao wanauza unga, wakikuona ni mteja wao wa kudumu na hubwii unga wanakuchanganyia katika bangi na matokeo yake unajikuta huwezi kuvuta bangi bila unga. Hivyo unakuwa teja bila kukusudia kama mimi nilivyochanganyiwa na mpenzi wangu katika sigara ya kawaida na kujikuta nakuwa teja

.
“Sasa wawe makini, hili halina mmoja licha ya baadhi yao kuwa chanzo cha kuwaingiza wasichana, lakini baadhi yao wanaweza kujikuta wanaingia huko kwa njia hiyo au kwa kugongeana sigara, yaani unamkuta rafiki yako anavuta na wewe unaomba akubakizie sasa kama alitia unga na wewe unaathirika.”
Msanii huyo alipoulizwa kuhusu mapenzi alisema; “Sina na nitakaa sana na hata nikiwa naye nitakuwa makini kwani nimeshang’atwa na nyoka kila nikiguswa na unyasi nashituka.”

No comments:

Post a Comment