KILA mchezaji wa Kitanzania hamu yake ni kucheza soka la
mafanikio nje ya nchi na hasa Ulaya kwa sababu akicheza huko atakuwa na
mafanikio makubwa na uchumi wake utakuwa.
Hiyo ni kutokana na imani kwamba klabu za Ulaya
zinalipa wachezaji fedha nyingi tofauti na zile za Tanzania.Henry
Joseph Shindika anakubaliana na hilo lakini anabainisha kwamba hawezi
kucheza soka Ulaya kwa sifa tu.
Henry nahodha wa zamani wa Simba na Taifa Stars
alikuwa anacheza soka ya kulipwa nchini Norway katika klabu ya
Kongsvinger aliyoichezea kwa miaka minne kuanzia 2009.
Lakini kwa wakati huu amerudi na kujiunga na
Simba, klabu aliyoichezea miaka ya nyuma jambo ambalo limewashtua
mashabiki wengi wa soka na wengine wamesikika wakiguna na kutilia shaka
kiwango cha Henry.
Katika mahojiano na Mwanaspoti, Henry anaeleza
mkasa mzima kuhusu sakata hilo hadi akatua Simba na si timu nyingine
yoyote kubwa kwenye ligi kama Yanga au Azam FC.
“Niliporudi hakuna klabu yoyote iliyonihitaji
zaidi ya Simba, ndiyo maana nikakubaliana nao na si timu nyingine, hata
hivyo ujio wangu hapa ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri kwenye ligi
na kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu waliopo, naamini tutairudishia
heshima yake kwa kuchukua ubingwa na vikombe vingine vilivyopo,”anasema.
Henry ametua kuichezea Simba, lakini maswali mengi
ya wadau wa soka ni kwa nini amerudi nchini wakati tayari alishapiga
hatua kwenye ligi zenye upinzani kama Norway.
“Najua wadau watakuwa na maswali mengi juu yangu
kwa nini nimerudi, lakini watambue kuwa sijapenda kurudi Tanzania
kirahisi isipokuwa ni mipango, tulishindana kwenye makubaliano kifedha,
ndiyo maana nikaona isiwe tabu, nirudi tu nyumbani niangalie mambo
mengine,” anasema.
“Kama unavyojua kucheza Ulaya kwa wachezaji kama
sisi, makato ya kodi ni makubwa, kwa hiyo siwezi kucheza huko kwa sababu
ni Ulaya kwa sifa tu wakati kiuchumi hakuna kitu.”
Henry alienda mbali na kuongeza kuwa kutokana na
makato hayo ingekuwa ngumu kwake kuishi huko: “Kuishi Ulaya ni gharama
lazima uwe na kazi nzuri inayokuingizia kipato kikubwa
kitakachokuwezesha kumudu kodi ambayo ni kubwa sana pamoja na gharama za
maisha kwa ujumla ziko juu.”
“Jambo hilo kwangu isingekuwa rahisi kwa haraka
haraka sawa na uraia ambao kuupata ni lazima uishi miaka mingi. Kurudi
kwangu Simba si kwamba nimekata tamaa, nina malengo mengi sana na mpango
wangu ni kutoka tena kwenda Ulaya kikubwa naomba uzima,” Henry anaeleza
kwa uchungu na kusisitiza maswali zaidi juu ya kisa chake aulizwe
meneja wake aliyemtambulisha kwa jina la Evance Malya.
Akitolea ufafanuzi, Malya anasema: “Unajua hili
suala la Henry kurudi Tanzania kubwa walishindindwana kimaslahi. Si
kwamba, ameshuka kiwango hapana, kama unavyojua msimu ule uliopita tu
alikuwa mchezaji bora kwenye timu isingekuwa jambo rahisi ashuke haraka
kihivyo.
No comments:
Post a Comment