Monday, September 23, 2013

SIMBA YAELEKEZA NGUVU ZAKE KWA JKT RUVU

Baada ya kutoka sare na timu ya mbeya city simba sports club inajiandaa na mchezo wake mgumu unaofuata dhidi ya Ruvu jkt.

Akizungumza na waandishi wa habari kocha msaisizi wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo "Julio" amesema kwamba wapokambini wanajiandaa  na mechi kali dhidi ya timu inayocheza mpira wa passi na wakasi ruvu jkt ambayo mnamo mwa mechi tatu za kwanza ilkuwa inaongoza ligi hiyo.

Aliongeza kwa kusema hakuna mtu asiyeijua timu ya ruvu jkt kwa kuwa inakua mechi ya ushindani dhidi yao na kila mtu kuhitaji kushinda mechi pindi wakikutana, lakini kwa wao wanajiandaa vizuri ili kushinda mechi hiyo na wameshaanza kurekebisha makosa yaliyotokea katika mechi iliyopita, hususan katika eneo la kiungo.

Mechi hiyo itakayofanyika jumapili itakuwa katika uwanja wa taifa na washabiki wote wa simba wanaombwa wafike kuisapoti timu yao ili wafanye vizuri katika mchezo huo japokuwa walitoka sare katika mchezo uliyopita.

No comments:

Post a Comment