Monday, September 23, 2013

BAADA YA KICHAPO DHIDI YA AZAM UONGOZI WA YAMGA WAOMBA RADHI MASHABIKI

Kufuatia kichapo kutoka kwa wana lambalamba Azam fc jana cha mabao 3-2,timu ya yanga kupitia kwa viongozi wake hatimaye wamewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo.

Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu leo aliwaoamba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya matokeo mabaya ya timu yao katika michezo ya ligi kuu ya hapa karibuni.

Yanga ilipata sare ya 1-1 na timu mbili za mkoani mbeya za prisons na mbeya city na jana katika uwanja wa taifa walifungwa mabao3-2 na timu ya Azam fc.

Kiongozi huyo alisema kwamba mashabiki wa timu hiyo wasiwe na wasiwasi na timu yao kwa matokeo hayo na hakuna mgogoro wowote ndani ya timu hiyo na kuwaasa au kuwaomba mashabiki hao kuendelea kuisapoti timu yao katika michezo yake ya ligi kuu inayoendelea.

No comments:

Post a Comment