Thursday, October 31, 2013

ROBINHO KUCHUKUWA NAFASI YA DIEGO COSTA BRAZIL

Nyota wa kimataifa wa Brazil Robinho anatarajiwa kuitwa na kocha wa taifa hilo Philipe Scolari ili kuziba pengo la Diego Costa.

Kocha huyo atamwita Robinho ili kujiandaa na michezo ya kirafiki ikiwemo dhidi ya chile hapo baadaye hasa baada ya kocha huyo kumuita nyota wa Athletico Madrid Diego Costa ambaye amekataa na kusema yeye anajiandaa na michezo katika taifa lake jipya na Hispania.

Robinho ataiwakilisha taifa hilo katika michezo ikiwemo kati ya Korea kusini na Zambia hapo baadaye.



LARS BENDER AJITIA KITANZI LEVERKUSEN NA KUWAKATISHA TAMAA ARSENAL

Kiungo mahiri wa timu ya taifa ya ujerumani na timu ya bayern leverkusen Las Bender hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuitumukia timu yake.

Nyota huyo mwenye miaka 24 ameingia mkataba mpya na timu yake ambao utamfikisha hadi mwaka 2019 katika kuitumikia timu hiyo.

Bender ambaye yupo katika rada za kocha wa Arsenal,  Wenger alikuwa na mkataba na timu hiyo hadi mwaka 2017 na sasa ameongeza miaka miwili baadaye.



FERGUSON AVUNJA REKODI NYINGINE

Kitabu cha Sir Alex Ferguson kimeweka rekodi ya kuwa kitabu kilichooza kwa haraka zaidi ndani ya Uingereza kikiuza nakala 115,547 katika siku chache za mauzo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Bookseller, kitabu hicho cha mocha wa zamani wa Manchester United kimevunja rekodi ya  Delia Smith,  ambaye kitabu chake cha mwaka 1999 cha mapishi kiliuza kopi 112,000 katika wiki take ya kwanza.

Pia kitabu cha Fergie kimevunja rekodi ya mauzo ya kitabu cha rafiki yake waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, ambacho kiliuza kopi 92,000 katika wiki ya kwanza.

VITABU VILIVYOUZA ZAIDI UK:
Sir Alex Ferguson - My Autobiography - 115,547
Delia Smith - How to Cook - book two - 112,000
Tony Blair - A Journey - 92,000
David Beckham - My Side - 86,000
Paul Burrell - A Royal Duty - 77,000

MALINZI AITWA NA BLATTER FIFA

RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter amemuambia rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwamba anakaribishwa wakati wowote FIFA anapotaka kujadili masuala yanayohusu mchezo huo. Pamoja na hayo, Blatter amesema ana uhakika ufahamu wake na uwezo wake katika uongozi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu nchini baada ya kushinda wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

 Blatter amempongeza Malinzi kwa kuchaguliwa na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake ya kuongoza mchezo huo nchini. “Nakutakia wewe na kamati mpya ya Utendaji iliyochaguliwa kila la kheri, nguvu, na kila aina ya mafanikio kwa changamoto zilizo mbele yenu,” amesema Rais Blatter katika salamu zake.

Wengine waliomtumia Rais Malinzi salamu za pongezi ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya, Rais wa Heshima wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arumeru (ADFA), Peter Temu.

Wakati huo huo: Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Novemba 1 mwaka huu) kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Tiketi zitauzwa siku ya mechi uwanjani katika magari maalumu kuanzia saa 4 asubuhi.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro). Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MECHI YA SIMBA VS KAGERA SUGAR YAMALIZIKA KWA MABOMU

UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam leo uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu hizo zikitoka 1-1.
  Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani.

Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi.
  Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mohamed Theofile wa Morogoro aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, ambao walishindwa kuumudu kabisa, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Baadhi ya viti vilivyong'olewa leo na mashabiki
 Kipa wa simba akiongea na mwamuzi wa akiba
 Baadhi ya wachezaji wa simba katika huzuni
 Shabiki wa simba akiwa chini ya ulinzi
 Sehemu ya jukwaa likionyesha jinsi viti vilinyotolewa
 Salum kanoni mwenye rasta akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli la kusawazisha kwa njia ya penalti

Wednesday, October 30, 2013

RAIS CAF AMPONGEZA JAMAL MALINZI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.

Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.

SIMBA KUJIULIZATENA KESHO MBELE YA KAGERA SUGAR

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.

YAYA TOURE ATEMBELEA KENYA

Mchezaji maarufu wa timu ya Manchester City Yaya Toure, amewasili mjini Nairobi Kenya kwa uzinduzi wa muungano mpya wa kukabiliana na uwindaji haramu kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP).
Muungano huo umeanzishwa ili kukabiliana na uwindaji haramu wa wanyama pori haswa Ndovu ambao wanakabiliwa na tisho la kudidimia kutokana na uwindaji haramu barani Afrika.
Toure, mshindi wa tuzo la mchezaji soka bora zaidi Mwafrika kwa miaka miwili mfululizo, 2011 na 2012 ataeleza kwanini amekubali kushirikiana na muungano huo kupambana dhidi ya uwindaji haramu na nini hasa jukumu lake.
Anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa mataifa katika mtaa w akifahari wa Gigiri, Nairobi.
Wengine watakao zungumza ni Achim Steiner mkurugenzi mkuu wa shirika la UNEP pampja na mkurugenzi wa shirikisho la kandanda la kenya Sam Nyamwea.


WAHISPANIA WAIUWA ARSENAL JANA KATIKA KOMBE LA LIGI

MABAO ya  Azpilicueta dakika ya 25 na Juan Mata dakika ya 66, jana usiku yameipa Chelsea ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal Uwanja wa Emirates, London katika mchezo wa Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One. 
KIkosi cha Chelsea kilikuwa: Schwarzer, Azpilicueta, Bertrand, Mikel, Cahill, David Luiz, De Bruyne/Ramires dk69, Essien, Eto'o/Ba dk81, Mata/Kalas dk90 na Willian.
Arsenal: Fabianski, Jenkinson, Monreal, Ramsey, Koscielny, Vermaelen, Miyaichi/Ozil dk63,  Wilshere, Bendtner/Giroud dk67, Rosicky na Cazorla.
J
 Jua Mata akiifungia goli timu yake
 Azplicueta akishangilia goli lake dhidi ya Arsenal
Wachezaji wa Arsenal akiwemo Ozil katikati wakitoka uwanjani baada ya mechi 

CHICHARITO APIGA MBILI UNITED IKIPATA NA USHINDI WA 4-0 DHIDI YA NORWICH CITY

MSHAMBULIAJI Javier Hernandez 'Chicharito' ameendeleza takwimu zake nzuri ndani ya Manchester United, licha ya kupewa nafasi chache za kucheza kwenye timu hiyo
Nyota huyo wa Mexico usiku wa jana amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 wa Manchester United dhidi ya Norwich katika Kombe la Ligi. 
Nyota huyo mwenye kipaji cha kufunga, alitikisa nyavu katika dakikaa 20 na 54 kwa penalti jana, wakati mabao mengine yalifungwa na Jones dakika ya 87 na Fabio dakika ya 90 na ushei.
Kikosi cha Man Utd jana kilikuwa: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Vidic, Büttner; Zaha/Rooney dk78, Cleverley/Anderson dk90, Jones, Young, Januzaj/Fabio dk90+3 na Hernandez.
Norwich: Bunn; Whittaker, R. Bennett, Bassong, Garrido; Snodgrass/Pilkington dk65, Fer, Johnson, Redmond/Murphy dk76, Hoolahan/Hooper dk89 na Elmander.
Chicharito akishangilia bao la kwanza 
Chicharito akifunga bao la pili
Wilfred Zaha alichezeshwa katika mechi yake ya kwanza katika mashindano
wachezaji wa united wakishangilia goli la tatu lililofungwa na Jones

Monday, October 28, 2013

WALKER ASAINI MKATABA MPYA SPURS

Beki wa kimataifa wa uingereza Kyle Walker hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo wa zamani wa Shielfe United alisaini akitokea clabuni hapo kwa ada ya uhamisho wa pauni millioni 8 mwaka 2009.

Lakini awali baada ya kusajiliwa alikwenda Ajilikwenda QPR na Aston villa kwa mkopo na baada ye kurudi ndani ya timu hiyo.

Walker amesaini mkataba wa muda mrefu  hasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri na timu tajiri kumtaka

SIMBA YACHEZEA KICHAPO CHA BAO 2-1 KUTOKA KWA AZAM

Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Azam FC, umemalizika kwa Simba kufungwa bao 2-1.
Mabao yote mawili ya Azam FC yalifungwa na Kipre Tchetche, mshambuliaji kutoka Ivory Coast.
Ramadhani Singano  ndie alieanza kuiweka Simba mbele kwa bao moja bila, kabla ya Kipre kuisawazishia bao moja na baadae kuongeza la pili la Ushindi.

Kwa matokeo hayo, Azam wanapanda nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 23.

Kapteni msaidizi wa timu ya simba Mganda Joseph Owino amesema kwamba ulikuwa ni mchezo mzuri ila haikuwa bahati yao kwa kuwa walicheza vizuri na kukosa nafasi nyingi katika mchezo huo na kuwa sisitiza mashabiki wa simba waskate tamaa na mchezo huu.

BAADA YA KUSHINDA URAIS TFF JAMAL MALINZI AVUNJA KAMATI ZOTE

Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.

Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.

Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).

Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni  Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).

Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.

Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).

Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).

Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).

Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).

Sunday, October 27, 2013

BREAKING NEWS: WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

STAA wa filamu nchini na Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Isaac Sepetu, amefiwa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu, aliyefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni mjini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa  matibabu.                 Balozi sepetu wakati akitibiwa TMJ

Habari zinasema kwamba, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital hiyo akipatiwa matibabu ya magonjwa ya Kiharusi na Kisukari yaliyokuwa yakimsumbua.

Balozi Isaac Sepetu amefariki akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. Pole Wema, pole familia ya marehemu ndugu na jamaa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin.

BREAKING NEWS: AZAM TV KURUSHA LIVE MICHUANO YA CHALLENGE MWEZI UJAO

MTENDAJI Mkuu wa Azam Media Group, Rhys Torrington amesema kwamba wanatarajia kununua haki za kuonyesha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge itakayofanyika mwezi ujao nchini Kenya.Torrington raia wa Uingereza alisema kwamba wapo katika mazungumzo na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) juu ya mpango huo.

 Kwa muda sasa, mashindano yote ya CECAFA yamekuwa yakionyeshwa na Televisheni ya SuperSport ya Afrika Kusini, lakini wamekuwa hawalipi chochote kwa madai eti wanapromoti soka ya ukanda huu, lakini Azam Media kupitia Azam TV wanataka kuweka fedha.
  Pamoja na mpango huo wa kuonyesha Challnge, Torrington alisema pia watakuwa wanaonyesha mashindano mengine makubwa ya kimataifa, ili kuwapa burudani zaidi watazamaji wake. 
      Huduma kamili za Azam TV zinatarajiwa kuanza rasmi mwezi ujao na kwa mujibu wa Rhys Torrington kila kitu knaendelea vizuri.

“Tutafungua milango ya Azam TV rasmi katikati ya Novemba kwa huduma ya chaneli 35 ambazo watu wajionea bure na uzinduzi utafanyika Novemba hiyo hiyo,”alisema.

Torrington alisema kwamba king’amuzi cha Azam TV kitauzwa kwa Sh. 95,000 pamoja na dishi lake na pia mteja kupatiwa huduma za kufungiwa na kuunganishiwa bure nyumbani kwake. Alisema malipo ya mwezi yatakuwa ni Sh. 12,500 tu na mteja atapata chaneli zaidi ya 50 katika king’amuzi cha Azam TV.

Alisema Azam TV pekee kwa kuanzia itakuwa na chaneli tatu ambazo ni Azam One itakayohusu habari za Afrika na zaidi za Kiswahili, Azam Two ambayo itakuwa ya kimataifa yenye vipindi mbalimbali duniani, na baadhi vya Kiswahili na Sinema Zetu itakayokuwa ikionyesha sinema za Kitanzania kwa saa 24 kila siku.

EXCLUSIVE: DARREN FLETCHER KURUDI DIMBANI DHIDI YA NORWICH CITY

Kiungo mahiri na mkakamavu wa Man United Darren Fletcher anatarajiwa kurudi dimbani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu dhid ya Norwich City katika kombe la capital one..

Nyota huyo raia wa Scotland alikaa nje zaidi ya miezi kadhaa tangu siku ya boxing day mwaka jana na anatarajiwa kurudi uwanjani ili kuimarisha safu ya kiungo cha timu hiyo.

Hata hivyo kiungo huyo hataonekana katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya kwani hakujumuishwa kama ni miongoni mwa wachezaji wataokuwepo katika ;ligi hiyo.

Kiungo huyo aarufu kama the sweeper mwnye miaka 29 alikuwa nje tangu timu yake ilipokutana na Newcastle ndani ya boxing day mwaka jana na atarudi wiki ijayo katika mchezo huo dhidi ya Norwich city.

INIESTA TAYARI KWA KUONGEZA MKATABA

Kiungo mahiri wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Andres Iniesta yupo tayari kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kipindi kingine.

Uongozi wa timu hiyo umebainiha kwamba utamuongeea mkataba nyota huyo hasa baada ya kuisaidia timu yake kutoka na ushindi dhidi ya Real Madrid jana.

Iniesta mwenye miaka 29 anatarajiwa kuongeza mkataba baada ya mkataba wake wa sasa kuishia mwisho wa msimu ujao waligi 2015.

"Nina furaha sana kwa ushindi wa leo hasa baada ya kumfurahisha kocha wetu Mortino kwani ni mchezo wake wa kwanza wa El classico na natumaini tutafanya vizuri zaidi chini yake na kwa sasa ninafuraha sana na nitaongeza mkataba siku zijazo"alsema Iniesta.

FABREGAS AELEZEA KWA NINI ALIKATAA KUJIUNGA MAN UNITED

Kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya hispania Cesc Faebrigas amesema kwamba alifanya jambo la usahihi kudharau kujiunga na mashetani wekundu wa Man United msimu wa usajili wa majira ya joto uliopita na kuendelea kubaki Barcelona.

Kocha wa United David Moyes alikuwa na nia ya kumsajili kiungo huyo lakini ikashindikana kutokana na Fabregas kukataa kujiunga na timu hiyo.

 Nyota huyo mwenye miaka 26 na kiungo wa zamani wa washika bunduki wa jiji la London Arsenal amesema kwamba mtu pekee aliyenisababisha kubaki ni kocha wake wa sasa Mortino ndiye aliyesababisha abaki na kumfanya aongezeke kiwango chake hadi hivi sasa.

"Ni kweli nilitaka kuiacha timu yangu na kutimkia ligi kuu ya ungereza lakini nikaamua moja tu ni kubakia katika clabu yangu hasa baada ya kuwasili kocha mpya na ninafuraha na najisikia mwenye kujiamini kila wakati" Fabregas alisema.

MATOKEO YA JANA LIGI KUU ENGLAND NA MSIMAMO WAKE

MATOKEO
26 October
 
Southampton2 - 0Fulham
St. Mary's Stadium
26 October
 
Aston Villa0 - 2Everton
Villa Park

26 October
 
Liverpool4 - 1West Bromwich Albion
Anfield
26 October
 
Manchester United3 - 2Stoke City
Old Trafford

26 October
 
Norwich City0 - 0Cardiff City
Carrow Road
26 October
 
Crystal Palace0 - 2Arsenal
Selhurst Park



MSIMAMO WA LIGI HIYO HADI HIVI SASA BAADA YA MICHEZO YA JANA 26 OCTOBER
PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Arsenal97112091122
2Liverpool9621178920
3Southampton9531103718
4Everton95311410418
5Chelsea8521145917
6Manchester City85122091116
7Tottenham Hotspur851285316
8Manchester United94231412214
9Hull City832379-211
10Newcastle United83231114-311
11Swansea City83141211110
12West Bromwich Albion9243810-210
13Aston Villa9315912-310
14Fulham9315912-310
15Cardiff City9234813-59
16West Ham United82248808
17Stoke City9225610-48
18Norwich City9225613-78
19Crystal Palace9108619-133
20Sunderland8017520-151

























TIMU YA WANAWAKE WA TANZANIA YAICHAPA MSUMBIJI 10-0

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa. Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.

Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa.
Kipindi cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona.
Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah. 
Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.

Tanzanites walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Dakika ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena, ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania bao la 10 dakika ya 90.
 
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel, Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa Yona.
Msumbiji; Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice Assane dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda Gove, Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na Onesema David. 

PICHA: BARCELONA VS REAL MADRID HUKU NEYMAR AKIWAUWA AKINA RONALDO KWA KUFUNGA GOLI LA KWANZA NA KUTOA PASI YA GOLI LA PILII

  wachezaji wa barcelona wakishangilia bao a kwanza alilofunga Neymar
 
NYOTA Mbrazil wa Barcelona, Neymar amekuwa na mwanzo mzuri katika mechi ya wapinzani wa jadi wa Hispania, 'El Clasico' baada ya kufunga bao katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Madrid leo.
Mambo yamekuwa tofauti kwa mchezaji ghali wa dunia, Gareth Bale ambaye alishindwa kuisaidia timu yake, Real Uwanja wa Nou Camp.
Bale alicheza kwa saa moja tu kabla ya kutolewa nje kipindi cha pili, ingawa alipambana sana na kufanikiwa kupiga mashuti kadhaa yaliyotoka nje ya lango la  Victor Valdes. 
Neymar alifunga dakika ya 19 na Alexis akaongeza la pili dakik ya 78, kabla ya Jese kuisawazishia Rela dakika ya 90.
 
 kipa wa Real Madid akiluka bila mafanikio na kufungwa bao la pili na Sanchez
 
Kikosi cha Barcelona: Valdés, Alves, Piqué, Mascherano, Adriano, Sergio Busquets, Xavi, Iniesta/Song dk77), Fàbregas/Alexis dk 70, Messi na Neymar/Pedro dk84.
Real Madrid: Diego López, Carvajal, Varane, Pepe, Marcelo, Ramos/Illarramendi dk56), Modric, Khedira, Di Maria/Jese dk76), Ronaldo, Bale/Benzema dk61.

 Cristiano ronaldo akilaumu jambo wakati wa mchezo
Gareth Bale akitafuta mbinu ya umtoka beki wa Barcelona Pique

Ronaldo na Bale wakishauriana jambo kabla ya kupiga faulo
 
makocha wa timu zote mbili wakifuatilia mcheo 


 messi akimtoka ronaldo jana wakati wa mchezo
 
 Rodroguez baada ya kuifungia madrid goli na kwanza