Monday, October 7, 2013

ASHLEY COLE KUIKOSA MONTENEGRO

Beki wa kushoto wa chelsea na timu ya taifa ya uingereza anataraiwa kuikosa mechi ya kimataifa dhidi ya montenegro baada ya kuumia katika mchezo kati ya chelsea na norwich jumapili iliopita.

Kutokana na kuumia kwa beki huyo mzoefu kunampa nafasi ya kucheza beki wa sehemu hiyo kutoka Arsenal Gibbs ambaye kwa muda mrefu hajaonekana katika kikosi hicho.
Vilevile mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya uingereza Wyne Rooney amesema kwamba timu hiyo itafuzu katika michuano ya kombe la dunia mwakani.

Hayo aliyasema baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na nafasi ya timu hiyo kupata nafasi kushiriki kombe hilo nchini Brazil, alisema ingawa katika timu yetu kila timu inanafasi ya kufuzu lakini aliipa nafasi timu yake kwa kuwa wako vizuri kushinda timu nyingine.

No comments:

Post a Comment