West Ham wametembeza kichapo dhidi ya Tottenham iliyotumia mabilioni kununua wachezaji wapya msimu huu.
Ravel Morrison ndiye aliyefunga bao la tatu na la ushindi kwa timu ya West Ham ilipoiadhibu Tottenham 3-0.Hakuna mtu aliyetarajia kwamba Tottenham wangechapwa namna hivyo hasa kwa kuzingatia kuwa ndiyo iliyovunja rekodi ya pesa nyingi za kuwanunua wachezaji wapya.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kimemalizika kwa timu mbili kutoshana nguvu kabla ya kijana Winston Reid kuingiza bao la kwanza kunako dakika ya 66 na Ricardo Vaz Te akafunga bao la pili dakia sita baadae.
Huo ni ushindi wa kwanza wa West Ham kwenye uwanja wa White Hart Lane tangu mwaka 1999 na ni ushindi wa kwanza wa ugenini tangu msimu huu kuanza.
Katika matokeo mengine Chelsea nao walipata ushindi ugenini kwa kuichapa Norwich mabao 3-1.Southampto waibugiza Swansea 2-0 na West Brom ilitoka sare na Arsenal ya bao 1-1.
Mechi ya mwisho jumamosi usiku ilishuhudia ushindi wa Manchester United wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Sunderland.
Arsenal bado kileleni.
Arsenal bado inakaa kileleni ikiwa na alama 17 sawa na Liverpool zikifwatiwa na Chelsea na Southampton zenye alama 14,huku Manchester City na Tottenham zikiwa na alama 13.Bingwa mtetezi Manchester United ni ya tisa na alama 10 na timu tatu za mwisho ni Norwich ,Crystal Palace na Sunderland.
No comments:
Post a Comment