Monday, October 21, 2013

BAADA YA KUWAONYESHA WATANI WAO WA JADI JINSI SOKA LINAVYOCHEZWA , SIMBA WAKO NJIANI KWENDA KUIKABILI COASTAL UNION TANGA

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu wa Tanzania bara maarufu kama vodacom primier league dhidi ya mahasimu wao wa jadi Yanga sc jana,  timu ya soka ya simba sc sasa ipo njiani ikielekea jijini Tanga kwa  ajili ya mchezo wao ligi kuu bara dhidi ya Coastal Union ya jijini hapo siku ya jumatano.

Katika mchezo wa jana simba iliionyesha maajabu na kuwafundisha mahasimu wao jinsi soka linavyochezwa na magoli yanavyoweza kurudi hata kama umeshinda magoli mia kipindi cha kwanza basi yawezekana kurudi magoli yote baada ya jana kurudisha magoli matatu na chupuchupu kuwafunga kutoka nyuma  baada ya kutanguliwa magoli matatu kipindi cha kwanza.

Pongezi ziende kwa makocha wawili wazawa Jamhuri Kihwelo "Julio" na kocha mkuu Abdallah Kibaden"Scolari" baada ya kuusoma mchezo kipindi cha kwanza na kuja kubadilisha mchezo kipindi cha pili na kurudisha bao zote.

Akizungumza kutoka njiani kuelekea Tanga kocha msaidizi wa timu hiyo amesema kwamba wachezaji wote wako vizuri na wapo tayari kuikabili timu hiyo ambayo inasadikika kuwa hatari ikiwa ndani ya uwanja wao wa nyumbani na ukizingatia imesheheni wachezaji ambao walishaichezea simba na timu zingine kumbwa ndani ya Afrika mashariki

No comments:

Post a Comment