Thursday, October 10, 2013

CHICHARITO AMUOMBA MOYES KUMPA MUDA ZAIDI WA KUANZA KIKOSI CHA KWANZA ILI KUONYESHA CHECHE ZAKE

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Mexico Javier Hernandez "chicharito" na timu ya manchester united amemuomba kocha wake David Moyes kumpa nafasi ya kuanza zaidi katika kikosi chake ili kuthibitisha thamani yake ndani ya timu hiyo.

Nyota huyo mwenye maka 25 ambaye alisajiliwa na united katika msimu wa 2010-2011 baada ya kung;ara katika mchuano ya kombe la dunia lililofanyika barani Afrika katika nchi ya Afrika kusini, akitokea timu ya Guadajala nchini Mexico.

Mshambuliaji huyo kwa sasa anawakati mgumu katika kikosi cha Moyes kutokana na kocha huyo kuwaamini zaidi Van Persie, Rooney, na Danny Welberck kuanza katika wakati tofauti katika safu ya ushambuliaji.

Kutokana na hayo chicharito amemuomba kocha wake kumpa muda zaidi na kumuonyesha kiwango cha katika kufumania nyavu, na ukifikiria hadi sasa ameshaanza mechi moja tu ambapo united walitoka na ushindi dhidi ya Liverpool kwa goli 1-0 lililofungwa na chicharito katika kombe la capital one.

Aliongeza kwa kusema kwa sasa anafuraha kubaki na timu hiyo na hana mategemeo yeyote kama ataondoka katika  kikosi hicho kwani anafurahia kucheza katika kikosi kilichosheheni wachezaji wenye vipaji na wa kiwango cha dunia kwani kila mchezaji anatamani kucheza katika timu kama hii, ila nita hakikisha ninacheza kwa nguvu zote ili kurudissha matumaini kwa kocha na kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.


No comments:

Post a Comment