Tuesday, October 22, 2013

HEMED MOROCCO AIACHA COASTAL UNION RASMI

Kocha kutoka visiwani Zanzibar Hemed Morocco ambaye miaka michache iliyopita hadi hivi karibuni alikuwa anaifundisha timu ya soka ya jijini Tanga inayoshiriki ligi kuu bara maarufu kama Vodacom primier league Coastal Union hatimaye ameiacha kuifundisha timu hiyo rasmi baada ya kutangaza leo.

Kocha huyo mwenye mafanikio na timu hiyo hivi karibuni ameifundisha timu hiyo  kwa kipindi kisichopungua miaka miwili baada ya kumaliza mkataba wake ambao ulikuwa unaisha october mosi mwaka huu na kwa mujibu wa tarehe hiyo tayari ameshamaliza mkataba huo na kutangaza kuiacha timu hiyo.

Awali ilifahamika baada ya kumalizika mkataba wake angeliongezewa mkataba mwingine lakini imesadikika kwamba imeshindikana kuongeza mkataba wa kuifundisha timu hiyo na badala yake anataka kupumzika kwanza.

Lakini swala hilo linaleta ali ya sitomfahamu kwani iweje watake kumpa mkataba na kushindikana na kwa hali hiyo inawapa maswali mengi washabiki wa soka kwani hivi karibuni inasadikika kwamba mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Nassor Binslum kujiweka kando na timu hiyo lakini bado haja fahamisha kwamba bado yupo au hayupo na timu hiyo.

Kiujumla hatutaki swala hili litokee kwenye timu hii kwani  ni miongoni mwa timu ambazo zilitakiwa kuleta ushindani katika ligi kuu msimu huu bada ya kusajili wachezaji wazuri na wenye uzoefu.

No comments:

Post a Comment