Saturday, October 5, 2013

IBRAHIMOVIC: NITAONDOKA KAMA PSG WAKISHINDWA KUNIAMINI

Mshambuliaji ghali wa timu ya PSG ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic amesema kwamba hawezi kuiacha timu hiyo labda mashabiki wa timu hiyo wakionyesha hali ya kuto mwamini.

Hayo aliyasema baada ya kuulizwa na chombo kimoja cha habari nchini Ufaransa na kusema kwamba kwa sasa ninafuraha kubwa kuichezea timu hiyo na sitarajii kuondoka.

Nyota huyo ambaye hivi karibuni ameongeza mkataba wa kuzidi kuitumikia timu hiyo na katikati mwa wiki aliiwezesha timu yake kutoka na ushindi dhidi ya Benfica ya ureno.

No comments:

Post a Comment