Monday, October 14, 2013

KUTOKANA NA KUJIANDAA NA MCHEZO WAO WA WATANI WA JADI, SIMBA , YANGA TAYARI ZAINGIA KAMBINI

Katika kujiandaa na mchezo wao wa jadi ambao utazikutanisha timu za simba na yanga katika uwanja wa taifa hapo jumapili tarehe 20 oktoba , tayari timu hizo zimeshaingia kambi kujiandaa na kipute hicho

Timu ya soka ya simba katika kujiandaa na mech hiyo ambayo huvuta hisia kwa washabiki wa soka nchini, tayari usiku huu wameelekea mjini Bagamoyo kuweka kambi hadi siku ya mechi itakapofika.

Kwa ujibu wa kocha msaidizi wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo "Julio" amesema kwamba timu ipo safarini ikiielekea Bagamoyo tayari kabisa kwa maandalizi na imekwenda na wachezaji wote tegemezi wakiwemo washambuliaji hatari Amis Tambwre na Mombeki.

Vilevile ameongeza kwa kusema kwamba wanamshukuru mwenyekiti wa  timu hiyo kwa kuwa karibu na maandalizi ya mchezo huwo na wapo nae safarini kueekea Bagamoyo wakitokea Bamba Beach ambako
 Simba waliweka kambi yao kabla.
 __________________________________________________________________________________




Nao mabingwa wa soka Tanzania bara wameelekea kisiwani Pemba tayari kwa maandalizi ya mchezo huo ambao huwa aina yake na kila timu huenda kukaa kambi sehemu inayohitaji tofauti na michezo mingine.

Kwa mujibu wa kocha msaidizi  wa Yanga, Fred Felix Minziro "Baba  Isaya" amesema kwamba timu hiyo ipo pemba na itakaa huko hadi  mechi itakapokaribia  na kusisitiza kwa kuwaomba mashabiki wa yanga waiombee dua timu yao katika maandalizi hayo huko kisiwani Pemba

No comments:

Post a Comment